Pata taarifa kuu

Mali : HRW yawashutumu wanajeshi na waasi kuwauwa raia

Nairobi – Makundi yenye silaha na wanajeshi wa Mali, wamewauwa raia wa kawaida 175 wengi wao wakiwa watoto, kati ya Aprili na Septemba mwaka huu, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch.

Utovu wa usalama, umeendelea kushuhudiwa tena Kaskazini mwa Mali, baada ya uongozi wa kijeshi kutaka kuondoka kwa wanajeshi wa UN
Utovu wa usalama, umeendelea kushuhudiwa tena Kaskazini mwa Mali, baada ya uongozi wa kijeshi kutaka kuondoka kwa wanajeshi wa UN © RFI
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo la Kimataifa la kutetea haki za binadamu, linaishtumu kundi la kijihadi kwa kutekeleza mauaji ya watu 135 katika mashambulio mawili katika kipindi hicho.

Aidha, kundi hilo lenye silaha mwezi Septemba, liliwaua watu 120 karibu na mto Niger, kwa mujibu wa wakaazi wa eneo hilo, huku jeshi la Mali na mamluki wa Urusi, wakituhumiwa kuwauwa raia 40.

Human Rights Watch, inasema imewasiliana na kuongoza wa kijeshi na kuwapa takwimu hizo, lakini hawajapata jibu huku uongozi huo ukishtumiwa kwa kuwalinda raia katika maeneo yenye utovu wa usalama.

Utovu wa usalama, umeendelea kushuhudiwa tena Kaskazini mwa Mali, baada ya uongozi wa kijeshi kutaka kuondoka kwa wanajeshi wa kulinda amani MINUSMA, ambao wanatarajiwa kuondoka kufikia mwisho wa mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.