Pata taarifa kuu

Wakenya kuathirika zaidi baada ya thamani ya Dola kupanda

Shilingi ya Kenya imeshuka thamani katika kiwango cha juu katika historia yake, ambapo sasa imefikia shilingi 150 dhidi ya dola ya Marekani, hali inayoongeza shinikizo kwa kupungua hifadhi ya fedha za kigeni huku uagizaji bidhaa ukiwa ghali zaidi kutokana na mfumuko wa bei.

Noti mpya za fedha nchini Kenya
Noti mpya za fedha nchini Kenya CBK
Matangazo ya kibiashara

Benki Kuu ya Kenya (CBK) imeweka kiwango cha ndani cha ubadilishaji dola kuwa shilingi 149.94, ikiwa ni poromoko la asilimia 24.

Aidha akiba ya fedha hadi Oktoba 19 ilifikia kiwango cha chini zaidi cha dola za Kimarekani bilioni 6.83, ambazo ziligharimu uagizaji wa bidhaa kutoka nje wa miezi 3.67, kushuka kutoka dola bilioni 7.29 mwaka mmoja uliopita.

Benki kuu, katika ripoti yake ya sekta ya fedha iliyotolewa Oktoba 15, ililaumu kudorora kwa sarafu ya nchi hiyo kutokana na "kuimarika kwa sera za kifedha katika mataifa yenye uchumi imara duniani hali ambayo ilifanya viwango vya riba vya kimataifa kupanda na kusababisha wawekezaji kukimbia kutumia sarafu imara kama dola ya Marekani.

CBK inakadiria kuwa ahueni katika mauzo ya nje, utatuzi wa mzozo wa Urusi na Ukraine, kuongezeka kwa fedha zinazotumwa kutoka nje ya nchi, uthabiti endelevu wa uagizaji bidhaa, kutachochea sarafu ya Kenya kurejea katika hali ya kawaida.

Katika hatua nyingine, mfumuko wa bei nchini humo uliongezeka kwa asilimia 6.8 mwezi Septemba, likiwa ni ongezeko la kwanza tangu Mei, kutoka asilimia 6.7 mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.