Pata taarifa kuu

Ubalozi wa Ethiopia jijini Khartoum umeshambuliwa

Balozi wa Ethiopia nchini Sudan amethibitisha kushambuliwa kwa ubalozi wa nchi yake jijini Khartoum kwa silaha nzito.

Zaidi ya watu 5,000 wameuawa katika mzozo huo na wengine milioni tano kukimbia makazi yao, kulingana na UN
Zaidi ya watu 5,000 wameuawa katika mzozo huo na wengine milioni tano kukimbia makazi yao, kulingana na UN REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa balozi wa Ethiopia nchini Sudan Yibeltal Ayimiro Alemu, hakuna majeruhi waliothibitishwa kwenye shambulio hilo japokuwa sehemu ya jengo la ubalozi huo iliharibiwa.

Wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF), ambao wamekuwa wakipagana dhidi ya jeshi la serikali tangu tarehe 15 ya mwezi April, wamevituhumu vikosi vya serikali kwa shambulio hilo.

Hadi tukichapisha taarifa hii, jeshi la taifa hilo la Afrika halikuwa limezungumzia shambulio hilo la siku ya Jumanne.

Hii sio mara ya kwanza kwa ubalozi wa Ethiopia jijini Khartoum kushambuliwa, pande mbili hasimu zikiendelea kutuhumiana kwa mashambulio hayo.

Mfanyakazi wa ubalozi wa Ethiopia nchini Sudan aliambia BBC kuwa ubalozi huo ulishambuliwa kwa mashambulio ya anga wiki tatu zilizopita na kumjeruhi mlinzi.

Zaidi ya watu 5,000 wameuawa katika mzozo huo na wengine milioni tano kukimbia makazi yao, kulingana na UN.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.