Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Niger: Jeshi lakumbwa na shambulio kubwa karibu na Kandadji

Shambulio kubwa la wanajihadi lilitokea asubuhi ya Alhamisi, Septemba 28 nchini Niger, katika eneo la mipaka mia tatu. Ngome ya jeshi iliyoko karibu na Kandadji, ambapo bwawa la kuzalisha umeme linajengwa, ililengwa. Kwa sasa hakuna hasara ambayo imetangazwa, lakini idadi ya askari kadhaa waliouawa imekuwa ikisambaa midomoni mwa watu.

Mwanajeshi wa Niger akiwa amesimama akishika doria, mnamo Septemba 10, 2021, karibu na eneo la ujenzi wa bwawa la kwanza ambalo nchi hiyo inajenga kwenye Mto Niger karibu na kijiji cha Kandadji, katika eneo la magharibi la "mipaka mitatu." » (Niger-Mali-Burkina Faso).
Mwanajeshi wa Niger akiwa amesimama akishika doria, mnamo Septemba 10, 2021, karibu na eneo la ujenzi wa bwawa la kwanza ambalo nchi hiyo inajenga kwenye Mto Niger karibu na kijiji cha Kandadji, katika eneo la magharibi la "mipaka mitatu." » (Niger-Mali-Burkina Faso). AFP - BOUREIMA HAMA
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mashahidi waliohojiwa na RFI, washambuliaji kadhaa waliokuwa kwenye pikipiki na kwenye magari walifanya shambulio dhidi ya ngome hii ya jeshi, na kusababisha mapigano makali, kulingana na chanzo cha usalama, na kuongeza kuwa wanajihadi walilazimika kutimka baada ya kuwasili kwa helikopta za kijeshi.

Idadi kubwa ya vikosi vya ulinzi ilitumwa katika eneo hilo, na operesheni ziliendeshwa hadi Tamalate, kijiji kilichoko upande wa mpaka wa Mali, kinachodhibitiwa na kundi la Islamic State katika eneo la Great Sahara (EIGS) tangu mwezi Machi 2022.

Ngome hii iliwekwa ili kuhakikisha usalama wa eneo kunakojengwa bwawa la Kandadji, kwenye Mto Niger, ambalo litakuwa bwawa kuu nchini, lakini shughuli zimesitishwa kwa sababu ya kusitiishwa kwa ufadhili wa kimataifa.

Vyanzo vya usalama vina wasiwasi kuona EIGS, ambayo hivi karibuni ilipanua maeneo inayodhibiti nchini Mali, ikitaka kufungua vita vipya upande wa Niger. Hasa tangu vitengo kadhaa jeshi linalopambana dhidi ya ugaidi, ikiwa ni pamoja na mamia ya vikosi maalum vilivyopewa mafunzo ya kupambana na wanajihadi, vimerudishwa Niamey kwa miezi miwili ili kuwalinda viongozi wa mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.