Pata taarifa kuu

Niger: Marekani 'itatathmini hatua zote' kuhusu uwepo wake kijeshi

Washington "itatathmini hatua zote katika siku zijazo" kuhusu uwepo wake wa kijeshi nchini Niger, baada ya tangazo la Ufaransa la kuwaondoa wanajeshi wake nchini humo mwishoni mwa mwaka, Waziri wa Ulinzi wa Marekani ametangaza leo Jumatatu.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin. REUTERS - EVELYN HOCKSTEIN
Matangazo ya kibiashara

"Tutaendelea kuzingatia hatua zozote za baadaye ambazo zitaweka kipaumbele malengo yetu ya kidiplomasia na usalama,” Lloyd Austin amesema katika mkutano na wanahabari katika mji mkuu wa KenyaNairobi, ambako anazuru.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza Jumapili hii jioni kwenye televisheni ya TF1 na France 2 kurejea nchini "katika saa zijazo" kwa balozi wa Ufaransa huko Niamey, na kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

'Hakuna tena ushirikiano kati ya Ufaransa na Afrika'

Uwepo wa Ufaransa nchini Niger, hata hivyo, umehalalishwa hadi sasa, kulingana na Emmanuel Macron "kwa sababu ya ombi la nchi kadhaa na kanda, tumekuwa tukipambana na ugaidi." Rais wa Jamhuri pia amekaribisha kujitolea kwa wanajeshi wa Ufaransa katika Operesheni Barkhane.

"Hakuna tena ushirikiano kati ya Ufaransa na Afrika, hatutaingilia kati wakati kunapotokea mapinduzi barani Afrika" hata hivyo ameongeza Emmanuel Macron.

Rais wa Ufaransa alitangaza katikati ya mwezi Septemba kwamba balozi wa Ufaransa nchini Niger alichukuliwa kama "mateka" na jeshi lililoko madarakani na alikuwa akila "mgao wa kijeshi". Viongozi hao wa mapinduzi, ambao walimpindua rais Mohamed Bazoum na kuchukua mamlaka mnamo Julai 26, waliagiza kufukuzwa kwa balozi wa Ufaransa mwishoni mwa mwezi Agosti, baada ya Paris kukataa kufuata makataa ya kumtaka aondoke. Hapo awali Ufaransa ilipinga kuondoka kwa balozi wake nchini Niger kwa wiki kadhaa, ikisema kuwa serikali iliyoko mamlakani haikuwa na mamlaka ya msingi ya kutoa ombi kama hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.