Pata taarifa kuu

Roger Whittaker, mwanamuziki maarufu mwenye asili ya Uingereza amefariki

Nairobi – Wakenya wanaomboleza kifo cha Roger Whittaker, mwanamuziki maarufu mwenye asili ya Uingereza, aliyezaliwa jijini Nairobi mwaka 1936. 

Whittaker, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87, akipatiwa matibabu Kusini mwa Ufaransa.
Whittaker, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87, akipatiwa matibabu Kusini mwa Ufaransa. AP - Eckehard Schulz
Matangazo ya kibiashara

Whittaker, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87, akipatiwa matibabu Kusini mwa Ufaransa. 

Wimbo wake uliopata umaarufu na kupendwa nchini Kenya, ni  My Land is Kenya( Kenya nchi yangu) aliouimba mwaka 1982. 

Wakenya huutumia wimbo huo wakati wa sherehe za uhuru na shughuli za taifa, kuonesha uzalendo. 

Wakati wa ujana wake Whittaker, alikuwa kwenye kikosi cha Ukoloni, kilichopambana na kundi la waasi la Mau Mau, lililokuwa linapigania uhuru, kabla ya kuondoka jeshini na kuwa Mwalimu. 

Atakumbukwa pia kwa kuwa na utaalam wa kuimba na kupiga gitaa pamoja na firimbi, na aliuza mikanda karibu Milioni 50 za kazi yake kote duniani. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.