Pata taarifa kuu

Ethiopia: Watu tisa waripotiwa kufariki baada ya kuambukizwa cholera

Watu tisa wamethibitishwa kufariki kutokana na mlipuko wa maambukizi ya ugonjwa wa cholera katika wilaya ya Benishangul-Gumuz kaskazini Magharibi wa Ethiopia.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kusambaa kwa maambukizo ya cholera katika maeneo 11 nchini Ethiopia tangu mwaka uliopita na kusababisha vifo vya watu 320
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kusambaa kwa maambukizo ya cholera katika maeneo 11 nchini Ethiopia tangu mwaka uliopita na kusababisha vifo vya watu 320 © AFP
Matangazo ya kibiashara

Vifo hivi vimethibitishwa na televisheni ya (ETV) inayomilikiwa na serikali ikiwanuku maofisa katika wizara ya afya kwenye taifa hilo.

Kwa mujibu wa Abdulmunhem Al-Beshir afisa katika wizara ya afya, karibia watu 131 waliambukizwa ugonjwa huo wakati wengine tisa wakifariki.

Visa vya maambukizo hayo vimeripotiwa katika wilaya tatu kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mamlaka ya afya katika wilaya Benishangul-Gumuz.

Haya yanajiri wakati huu maambukizo ya cholera yakiripotiwa kusababisha vifo vya raia tisa wa Sudan ambao ni wakimbizi katika jimbo la Amhara kaskazini Magharibi mwa Ethiopia.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kusambaa kwa maambukizo ya cholera katika maeneo 11 nchini Ethiopia tangu mwaka uliopita na kusababisha vifo vya watu 320.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka miwili na ukame yamechangia katika mzozo wa kibinadamu katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.