Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Utawala wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger waelekea kwenye ushirikiano wa kiusalama

Bamako, Ouagadougou na Niamey wametia saini mkataba wa Liptako-Gourma Jumamosi hii, Septemba 16. Mkataba huo umetiwa saini na wakuu wa tawala tatu za kijeshi, nakala hiyo itapelekea kuundwa kwa chombo kipya: Muungano wa nchi za Sahel, kwa lengo la kuunda mifumo ya ulinzi wa pamoja na usaidizi wa pande zote.

Kapteni Ibrahim Traoré, kiongozi wa utawala wa kijeshi (katikati), amekutana na viongozi wenzake wa Mali na Niger kwa minajili ya kutia saini makubaliano ya ushirikiano.
Kapteni Ibrahim Traoré, kiongozi wa utawala wa kijeshi (katikati), amekutana na viongozi wenzake wa Mali na Niger kwa minajili ya kutia saini makubaliano ya ushirikiano. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Ni hatua katika historia inayochipukia ya tawala tatu za kijeshi zilizochukua mamlaka hivi karibuni nchini Mali, Burkina Faso na Niger. Jumamosi hii, Septemba 16, viongozi wa kijeshi wa kila nchi, Kanali Goïta, Kapteni Traoré na Jenerali Tiani, walikutanakwa minajili ya  kutia saini kwenye kataba wa Liptako-Gourma.

Nchi hizi tatu zimejikubalisha kusaidiana iwapo kutatokea shambulio dhidi ya mamlaka na uadilifu wa nchi zao. Lengo ni kuunda muungano mpya, Muungano wa Nchi za Sahel, pamoja na mifumo ya ulinzi. Katika tukio la kitendo ambacho kinaweza kuchukuliwa kama uchokozi, wanachama wengine lazima watoe usaidizi na uokoaji. Lakini juu ya yote, wataweza kutumia jeshi "ikiwa ni lazima".

Ushirikiano pia unahusu mapambano dhidi ya ugaidi, uhalifu uliopangwa, lakini pia uasi wa kutumia silaha. Ikiwa inasemekana kuwa njia ya amani inapendelewa, matumizi ya nguvu yanaonyeshwa tena kama uwezekano. Msaada huu wa pande zote unatumika katika tukio la shambulio dhidi ya vikosi vya usalama, meli na ndege za nchi wanachama, katika nchi wanachama, lakini pia nje ya nchi.

Maandamano ya kuvitaka vikosi vya Ufaransa kuondoka

Kwa mkataba huu, tawala tatu za kijeshi zinaimarisha zaidi ushirikiano wao. Mnamo Julai 31, walikuwa tayari wamekataa kutekeleza vikwazo vya ECOWAS dhidi ya Niger, wakiviona kuwa ni "kinyume, haramu na zisizo za kibinadamu". Nchi hizo tatu zilionya kwamba uingiliaji kati wa kikanda wenye silaha utazingatiwa kama tangazo la vita. Tarehe 24 Agosti, Niamey ilitia saini amri zinazoidhinisha wanajeshi wa Mali na Burkinabe kuingilia kati nchini Niger katika tukio la uvamizi.

Wakati huo huo, maelfu ya vijana wa Niger wanaounga mkono jeshi lililo madarakani huko Niamey waliandamana tena kwa lengo la kujaribu kuvishinikiza vikosi vya Ufaransa kuondoka. Maandamano hayo, yaliyoandaliwa na Kamati ya Kusaidia viongozi wa mapinduzi, kwanza yalianza kama mkutano katikati mwa jiji. Kisha maandamano kuelekea uwanja wa ndege, ambapo vikosi vya kijeshi vya kigeni vinapatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.