Pata taarifa kuu

Sudan: Mashirika ya kiraia yatiwa hofu na vita na hali ya kibinadamu

Nchini Sudan, wanajeshi wa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, kamanda wa jeshi, wanakabiliana na vikosi vya Jenerali Hemedti, vikosi vya msaada wa haraka. Jumatano hii asubuhi, mashirika 50 ya kibinadamu na haki za binadamu yametoa taarifa ya pamoja kuuomba Umoja wa Mataifa kujikita zaidi katika mgogoro huu ambao wanauelezea kama "janga" la kibinadamu.

Watu wamesimama kwenye vifusi walipokuwa wakikagua nyumba iliyoshambuliwa kwa kombora katika wilaya ya Azhari, kusini mwa Khartoum, Juni 6, 2023.
Watu wamesimama kwenye vifusi walipokuwa wakikagua nyumba iliyoshambuliwa kwa kombora katika wilaya ya Azhari, kusini mwa Khartoum, Juni 6, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo mgogoro wa Sudan umekuwa ajenda kwa miongo kadhaa, bado halijapitisha azimio moja la msingi la kukabiliana na mzozo uliopo," imeandikwa katika taarifa ya mashirika hayo 50 yasio kuwa ya kiserikali.

Mashambulizi, unyanyasaji wa kijinsia, kukamatwa kiholela na mauaji… orodha ya ukiukaji wa haki za binadamu ni ndefu. Na mzozo sasa unaendelea huko Khartoum, Kordofan Kusini na Jimbo la Blue Nile.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, Wasudan milioni 20 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, ikiwa ni pamoja na milioni 6 kutokana na njaa na karibu watoto 500 tayari wamekufa kwa njaa. "Raia wa Sudan wanakabiliwa na mzunguko usio na mwisho wa vifo na uharibifu," amesema Agnès Callamard, Katibu Mkuu wa shirika la kimataifa la haki za Bunadamu la Amnesty International.

Wikendi mbaya hasa

Wakati huo huo, mashirika 26 yasio kuwa ya kiserikali kutoka Marekani pia yameomba baraza la Congress kusikiliza mashirika ya kiraia ya Sudan, ili "kupitia upya msimamo wa Marekani" juu ya mgogoro huu.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa siku ya Jumanne, shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) wanadai kuwa walishuhudia wikendi yenye umwagaji mkubwa wa damu tangu kuanza kwa mzozo huo. Watu 49 waliuawa na mia kujeruhiwa katika shambulio la bomu katika soko moja katika mji mkuu, Khartoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.