Pata taarifa kuu

Sudan: Jenerali Abdel Fattah al-Burhan anazuru Misri

Nairobi – Kiongozi wa jeshi nchini Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesafiri kuelekea nchini Misiri, hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuanza kwa mapigano mwezi Aprili.

Jenerali huyo anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Misiri Abdel Fattah al-Sisi
Jenerali huyo anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Misiri Abdel Fattah al-Sisi © ASHRAF SHAZLY/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inakuja wakati huu machafuko ya kikabila yakiendelea kuripotiwa katika eneo la Darfur ambako mamia ya raia wamethibitishwa kuwaua.

Kiongozi huyo ameondoka nchini humo wakati huu pia wahudumu wa afya wakisema kwamba raia 39 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wameuawa katika shambulio katika mji wa Nyala, mji mkuu wa pili wa Sudan kuisini mwa jimbo la Darfur ambapo mapigano kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF yameshika kasi.

Jenerali huyo anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Misiri Abdel Fattah al-Sisi, mshirika wake muhimu kuhusu utatuzi wa mzozo unaoendelea nchini mwake.

Mapigano kati ya jeshi linaloongozwa na Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, ambaye sasa ni mpizani wake mkuu yamekuwa yakiripotiwa tangu mwezi Aprili tarehe 15 ya mwaka huu.

Vita hivyo kwa sasa vimesambaa kutoka katika mji mkuu wa Sudan Khartoum hadi katika maeneo mengine ya Magharibi mwa Darfur kuelekea Kordofan na jimbo la Jazira, ambapo maelfu ya raia wameuawa mamilioni yaw engine wakiwa wametoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.