Pata taarifa kuu

Arobani na sita wauawa katika mashambulizi ya anga Khartoum, jeshi lakanusha kuhusika

Jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, ambalo linatumia ndege za kivita katika mzozo huu, limekanusha kuhusika na shambulizi la anga, baada ya kundi hasimu kulishtumu kwa mauaji ya watu 46.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilisema jumuiya ya Afrika nzima "haipaswi kutoa nafasi kwa vuguvugu la waasi au wanamgambo wa kigaidi".
Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilisema jumuiya ya Afrika nzima "haipaswi kutoa nafasi kwa vuguvugu la waasi au wanamgambo wa kigaidi". © Mohamed Nureldin Abdallah / RFI
Matangazo ya kibiashara

Tangu Aprili 15, vita vya kugombea madaraka nchini Sudan kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo vimesababisha vifo vya watu 7,500 na karibu milioni tano kuyahama makazi yao na wakimbizi wa nadani, kulingana na shirika moja lisilo la kiserikali.

Idadi halisi kwa kweli ni kubwa zaidi ya hiyo iliyotangazwa kwa sababu maeneo mengi ya nchi hayaingiliki, hasa Darfur (magharibi), na kambi hizo mbili zinakataa kutangaza hasara wanazopata katika vita hii.

Kulingana na moja ya makundi yanayounga mkono demokrasia ambayo yanatoa misaada ya pande zote kati ya wakazi, mashambulizi ya mabomu "yaliyofanywa na ndege za kijeshi" yalilenga wilaya ya Quuro, kusini mwa Khartoum.

Shambulizi hili "lilifanywa mwendo wa 7:15 asubuhi siku ya Jumapili (saa za Suadan) kwenye soko," imesema kamati hiyo huko Qouro, ikilaani "mauaji."

"Leo asubuhi wanamgambo wa kigaidi wa Burhane walifanya mashambulizi ya anga dhidi ya raia kusini mwa Khartoum," ilisema taarifa ya FSR kwenye X, mtandao wa zamani wa Twitter.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kupitia shirika la serikali la Suna, jeshi la Jenerali Burhane lilikanusha kuhusika na "mashambulio ya anga yaliyolenga raia" huko Qouro na kufutilia mbali"madai ya uwongo yasiyo kuwa na msingi ya waasi (FSR)".

Idadi ya vifo sasa imefikia "angalau 40", wanaharakati wanasema. Hata hivyo, wanasema wanahofia kuongezeka kwa idadi kubwa zaidi wakati "watu waliojeruhiwa bado wanawasili katika hospitali ya Bachaïr".

Uhusiano umedorora kati ya jeshi na Umoja wa Afrika (AU) baada ya mkutano wa wiki jana kati ya mmoja wa viongozi wake na afisa wa RSF.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilisema jumuiya ya Afrika nzima "haipaswi kutoa nafasi kwa vuguvugu la waasi au wanamgambo wa kigaidi".

Na siku ya Jumamosi, Jenerali Burhane alisema "hatahitaji usaidizi" kutoka AU ikiwa umoja huo hautabadilisha mtazamo wake.

Sudan ilisimamishwa AU kufuatia mapinduzi ya mwaka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.