Pata taarifa kuu

Sudani: Mvutano na vurugu vyaongezeka al-Jazirah

Al-Jazirah, jimbo la tatu kwa idadi kubwa ya watu nchini Sudan, liko chini ya hali ya tahadhari: tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, makabiliano yameongezeka katika jimbo hilo kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Mabadiliko ya hivi majuzi ya utii wa wanamgambo wa ndani pia yanazua hofu. Kufikia sasa, mji mkuu wa jimbo hilo, Wad Madani, umekuwa kimbilio la wakazi wengi wa Khartoum waliokimbia vita vilivyoanza Aprili 15.

Malori na magari mengine yakiwa yameegeshwa kando ya barabara inayounganisha mji mkuu wa Sudan na mji wa Wad Madani katika jimbo la al-Jazirah, huko Hasahisa, Julai 18, 2023.
Malori na magari mengine yakiwa yameegeshwa kando ya barabara inayounganisha mji mkuu wa Sudan na mji wa Wad Madani katika jimbo la al-Jazirah, huko Hasahisa, Julai 18, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Nchini Sudan, wakaazi wa al-Jazirah, iliyoko viungani mwa mji wa Khartoum, wanaelezea hofu yao kwamba mapigano hayo yataenea hadi jimboni mwao. Wad Madani, mji mkuu wa jimbo hilo, ulioko kilomita 200 kusini mwa mji mkuu wa Sudan hadi sasa umeepushwa na mapigano hayo. Jiji hili pia limepokea idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao kutoka Khartoum.

Wanamgambo wajitenga na jeshi na kujiunga na kikosi cha RSF

Wasiwasi huo unaonekana wazi katika mji wa Wad Madani, ambao unakabiliwa na tishio la FSR. Wiki iliyopita, wanamgambo wa ndani 'ngao' walijitenga na jeshi na kujiunga na RSF. Wanamgambo hawa, ambao wana idadi ya maelfu ya wapiganaji, wanaongozwa na Abou Akla Kikel. Msimamo wake ulishangaza kila mtu na kuwatahadharisha wenyeji na jeshi.

Kwa msaada huu, RSF ilijaribu kushambulia Wad Madani, lakini walizuiwa na mashambulizi ya anga ya jeshi. Mapigano yalitokea kwenye barabara inayoelekea Wad Madani.

Kulingana na gavana wa al-Jazirah, RSF pia ilifanya uvamizi kaskazini mwa jimbo hilo na mapigano yalitokea na wenyeji katika vijiji kama al-Noba, kilichoshambuliwa mara mbili.

Jeshi liliongeza hatua za usalama karibu na Wad Madani kwa kuimarisha vituo vya ukaguzi na kumkamata yeyote anayeshukiwa kuunga mkono RSF huko al-Jazirah. Miongoni mwa waliokamatwa, wauzaji chai au wakimbizi kutoka magharibi mwa Sudan. Amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa Wad Madani. Katika jimbo la al-Jazirah, karibu vijana 15,000 wa kujitolea wameingia katika kambi za mafunzo ya jeshi, kulingana na vyanzo vya kikabila.

Kwa kuongezea, shughuli yoyote ambayo jeshi halipendi ni marufuku katika jiji. Chama cha wanawake, ambacho kilikuwa kikiandaa kongamano dhidi ya vita hivyo, kilipigwa marufuku na waandalizi kuhojiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.