Pata taarifa kuu

Marekani 'yapanga upya' wanajeshi wake nchini Niger

Marekani imeanza 'kama tahadhari' kupanga upya wanajeshi wake nchini Niger, nchi iliyoshuhudia mapinduzi ya kijeshi mwishoni mwa mwezi Julai, Pentagon imetangaza siku ya Alhamisi usiku.

Marekani ina wanajeshi 1,100 walioko Niger, ambao wamekuwa wakiendesha operesheni zao dhidi ya makundi ya kijihadi yanayoendesha harakati zao katika eneo hili.
Marekani ina wanajeshi 1,100 walioko Niger, ambao wamekuwa wakiendesha operesheni zao dhidi ya makundi ya kijihadi yanayoendesha harakati zao katika eneo hili. AFP - CHRISTOF STACHE
Matangazo ya kibiashara

Idara ya Ulinzi "inapanga upya sehemu ya wafanyakazi wake na vifaa vyake kutoka kituo cha anga cha 101 huko Niamey, mji mkuu wa Niger, kwenda kituo cha 201 huko Agadez", kaskazini, mmoja wa wasemaji wake, Sabrina Singh, amewaambia waandishi wa habari.

"Hakuna tishio limeshatokea kwa wafanyakazi wetu au chokochoko yoyote dhidi yao," ameongeza, akiita uamuzi huo "hatua ya tahadhari."

Bi Singh pia amesema kwamba "baadhi ya wafanyakazi wasio wa lazima na wakandarasi" waliondoka nchini wiki kadhaa zilizopita.

Wanajeshi walimpindua Rais wa Niger Mohamed Bazoum mnamo Julai 26 na kumweka yeye na familia yake katika kizuizi cha nyumbani katika ikulu ya rais.

Marekani ina wanajeshi 1,100 walioko Niger, ambao wamekuwa wakiendesha operesheni zao dhidi ya makundi ya kijihadi yanayoendesha harakati zao katika eneo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.