Pata taarifa kuu
USULUHISHI-USHIRIKIANO

China kuchukua 'jukumu la upatanishi' katika mgogoro wa Niger

Serikali ya China inakusudia kuchukua "jukumu la upatanishi" katika mzozo wa kisiasa nchini Niger, ametangaza balozi wa China nchini humo katika mahojiano Jumatatu usiku kwenye televisheni ya taifa ya Niger.

Raia hawa waandamana wakishikilia bendera za Nigr na Urusi, huko Niamey, mji mkuu wa Niger.
Raia hawa waandamana wakishikilia bendera za Nigr na Urusi, huko Niamey, mji mkuu wa Niger. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Serikali ya China inakusudia kuchukua jukumu la mpatanishi, kwa heshima kamili kwa nchi za kikanda kwa minajili ya kutafuta suluhisho la kisiasa la mzozo huu wa Niger," amesema balozi huyo katika mahojiano haya, baada ya mkutano na Waziri Mkuu wa Niger Ali Mahaman Lamine Zeine, aliyeteuliwa na wanajeshi waliochukua madaraka.

"China inafuata kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine" na kuhimiza nchi za Afrika "kutatua matatizo yao kwa njia amani kupiia wao kwa wao," balozi huyo ameongeza.

China ni mshirika mkuu wa kiuchumi wa Niger, hasa katika sekta ya nishati.

Nchi hizo mbili zinajenga bomba la mafuta la kilomita 2,000, refu zaidi barani Afrika, linalokusudiwa kusafirisha mafuta ghafi kutoka mashamba ya Agadem (kusini-mashariki mwa Niger) hadi bandari ya Sèmè nchini Benin.

Visima vya mafuta vya Agadem vinatumiwa na kampuni ya mafuta ya China National Petroleum Corporation (CNPC), ambayo pia imejenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Zinder, kusini mwa Niger, chenye uwezo wa kubeba mapipa 20,000 kwa siku na kampuni hiyo ya China ina asilimia kubwa ya hisa katika kiwanda hiki.

Makampuni ya China pia yanafanya kazi ya ujenzi kwenye bwawa la Kandadji kwenye Mto Niger, mradi wa pharaonic wenye thamani ya faranga za CFA bilioni 740 (sawa na euro bilioni 1.1) ulioko magharibi mwa nchi, ambao unapaswa kuzalisha GWh 629 kila mwaka ili kuwezesha Niger kujikomboa kutoka kwa utegemezi wake wa nishati kwa nchi jirani ya Nigeria.

Kufuatia mapinduzi hayo, Nigeria ilikata usambazaji wake wa umeme nchini Niger, kulingana na vikwazo vilivyoamuliwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.