Pata taarifa kuu

Mwanasoka wa Mali na Mchezaji wa Zamani wa Saint-Étienne Salif Keita, aaga Dunia

NAIROBI – Mchezaji wa zamani wa kandanda wa Mali, Salif Keita, amefariki Dunia Jumamosi mjini Bamako akiwa na umri wa miaka 76, Waziri wa Michezo wa Mali amethibitisha taarifa hiyo. 

Salif Keita, kushoto, akimchenga Simon Rolfes wa Leverkusens wakati wa mechi ya shirikisho la soka la Ujerumani ya Kombe la DFB kati ya mchezaji wa daraja la 2, kwenye uwanja wa Koblenz, Jumamosi, Septemba 9, 2006.
Salif Keita, kushoto, akimchenga Simon Rolfes wa Leverkusens wakati wa mechi ya shirikisho la soka la Ujerumani ya Kombe la DFB kati ya mchezaji wa daraja la 2, kwenye uwanja wa Koblenz, Jumamosi, Septemba 9, 2006. AP - HERMANN J. KNIPPERTZ
Matangazo ya kibiashara

Salif Keita ni Mshindi wa kwanza wa tuzo ya Ballon d’Or ya Afrika mwaka wa 1970 na alianza soka lake nchini Mali katika klabu ya Real Bamako. 

Bingwa huyu pia alizichezea klabu kubwa katika ligi ya Ufaransa Saint-Étienne na Marseille katika miaka ya 1970. 

Mshambulizi huyu wa zamani wa Mali aliwahi kuhudumu serikalini kama mjumbe wa Waziri Mkuu aliyesimamia mpango wa kibinafsi katika serikali ya mpito ya Mali (1991-1992).  

Pia aliongoza shirikisho la soka nchini humo Femafoot katika miaka ya 2000. 

Akiwa na umri wa miaka 17 aliitwa katika timu ya taifa ya Mali baada ya kucheza mechi chache sana katika ligi kuu nchini Mali. 

Akiwa na umri wa miaka 23 alisafiri kuenda ufaransa hili kujiunga na Saint-Étienne maarufu The Greens na kua bingwa wa Ufaransa mara tatu (1968, 1969, 1970) na mshindi mara mbili wa Coupe de France (1968, 1970) kabla ya kuondoka kwenda Marseille mnamo 1972. 

 

Salif hakutamba Ufaransa pekee bali pia Hispania alikochezea Valencia na Ureno akiitumikia Sporting Cp kabla ya kumaliza kazi yake nchini Marekani, huko Boston. 

Mnguli huyu wa soka pia aliigiza katika filamu "Le Ballon d'Or", iliyochochewa kwa uhuru na hadithi yake. 

Alipewa jina la utani "Domingo" na marafiki zake kwa kurejelea jina lililoonekana kwenye alama za bango la sinema alipokuwa na umri wa miaka kumi. 

Kimwili Salif Keita alikua mchezaji mwembamba, mwenye mbinu isiyo na kifani ya kuufanyia mpira chochote alichofikiria uwanjani. 

Gwiji huyu amefariki siku ambayo AS Saint-Etienne ilipaswa kumuenzi gwiji mwingine wa klabu, George Bereta, ambaye alifariki mwanzoni mwa majira ya kiangazi, wakati wa mechi ya Ligue 2 ASSE-Valenciennes. 

Absou Kassim Ibrahim Fomba na shirikisho la soka nchini Mali ni baadhi ya waliotoa jumbe za rambirambi. 

Salif ambaye ni mtoto wa dereva wa Lori pia ni mjombake mchezaji wa zamani wa Barcelona na timu ya Mali Seydou Keita. 

Kando na kulisaidia taifa la mali katika ukuzaji wa vipaji anakumbukwa sana kwa safari yake kuenda kujiunga na klabu ya saint Entienne akitoka katika jiji la Paris kwa teksi. 

Lichomozapo jua lazima litatua na mwisho wa kila kiumbe chenye Uhai duniani ni Mauti. Rambirambi kwa jamaa na familia ya mpira wa miguu. 

Ripoti yake mwanaspoti wa RFI Kiswahili Paul Nzioki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.