Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Afrika Kusini: Watu 18 wauawa na polisi kwa kupigwa risasi

Watu 18 waliuawa na polisi siku ya Ijumaa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Limpopo kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini, huku polisi wakisema waliwalenga washukiwa waliotaka kuiba gari la kusafirisha pesa.

Mwaka jana, washukiwa kumi waliokuwa wakijaribu kuteka nyara usafiri wa pesa waliuawa baada ya kufyatulia risasi helikopta ya polisi na kumjeruhi rubani, jambo lililosababisha majibu ya polisi.
Mwaka jana, washukiwa kumi waliokuwa wakijaribu kuteka nyara usafiri wa pesa waliuawa baada ya kufyatulia risasi helikopta ya polisi na kumjeruhi rubani, jambo lililosababisha majibu ya polisi. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Mara tu polisi walipokaribia, kundi la washukiwa lilianza kufyatua risasi na polisi walijibu. Wanaume kumi na sita na wanawake wawili walikufa papo hapo," polisi ya Afrika Kusini imsema katika taarifa.

Afisa wa polisi "alijeruhiwa vibaya sana", Fannie Masemola, kamishna wa polisi huko Makhado, katika jimbo la Limpopo, lililoko takriban kilomita 430 kaskazini mashariki mwa Johannesburg, amewaambia waandishi wa habari.

Makabiliano kati ya washambuliaji hao na polisi  yalidumu saa moja na nusu, amesema.

Kwa mujibu wa polisi waliokuwa wakifuatilia washukiwa hao kwa siku kadhaa, uchunguzi ulifunguliwa mwezi Januari kwa usaidizi wa idara za upelelezi.

"Nia yetu ilikuwa kuwakomesha kabla hawajafanya uhalifu wao," amesema.

Mwaka jana, washukiwa kumi waliokuwa wakijaribu kuteka nyara usafiri wa pesa waliuawa baada ya kufyatulia risasi helikopta ya polisi na kumjeruhi rubani, jambo lililosababisha majibu ya polisi.

Mwezi Mei, Waziri wa Polisi Bheki Cele aliripoti ongezeko la 20% la mashambulizi dhidi ya magari ya kusafirisha pesa, huku kesi 64 zikirekodiwa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka.

Takwimu za uhalifu, zinazowasilishwa na waziri huyo moja kwa moja kwenye televisheni kila baada ya miezi mitatu, zimeongezeka katika miezi ya hivi karibuni katika nchi ambayo inarekodi moja ya viwango vya juu zaidi vya uhalifu duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.