Pata taarifa kuu

Watu 63 wameuawa katika ajali ya moto kwenye jengo Afrika Kusini

Nairobi – Takriban watu 63 wameuawa na zaidi ya 40 wakiachwa na majeraha kufuatia moto kwenye jengo la ghorofa nyingi katikati mwa jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani na mfanyakazi wa dharura.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya mtandaoni ya News24 ya Afrika Kusini.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya mtandaoni ya News24 ya Afrika Kusini. REUTERS - SIPHIWE SIBEKO
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa huduma za dharura za Johannesburg Robert Mulaudzi amesema moto huo uliotokea Alhamisi asubuhi uliteketeza jengo lililoko katikati mwa jiji la kibiashara, na idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka huku miili 63 ikipatikana kutoka eneo hilo kufikia sasa tunapochapisha taarifa hii.

Inaelezwa kuwa angalau mtoto mmoja alikuwa miongoni mwa waliofariki, na wale waliojeruhiwa katika moto huo wanapokea matibabu katika vituo mbalimbali vya afya.

Chanzo cha moto huo bado hakijabainika
Chanzo cha moto huo bado hakijabainika AP

Mulaudzi alisema jengo hilo lilikuwa "makazi yasiyo rasmi" ambapo watu wasio na makazi wamehamia kutafuta makao bila makubaliano yoyote rasmi ya kukodisha. Alisema hilo lilifanya iwe vigumu kwa waokoaji kupekua jengo hilo.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya mtandaoni ya News24 ya Afrika Kusini.

Moto huo kwa kiasi kikubwa ulizimwa, kulingana na mamlaka
Moto huo kwa kiasi kikubwa ulizimwa, kulingana na mamlaka AP

Moto huo kwa kiasi kikubwa ulizimwa, kulingana na mamlaka, lakini moshi ulionekana ukitoka kwenye madirisha ya jengo hilo lililokuwa na rangi nyeusi katikati mwa jiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.