Pata taarifa kuu

Mazungumzo ya kuijumuisha Somalia kuwa mwanachama wa EAC yameanza

Nairobi – Mazungumzo ya kuijumuisha Somalia kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, yameanza jijini Nairobi. Iwapo nchi hiyo itafanikiwa itakuwa nchi ya nane kujiunga baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki http://eac.int/
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya Somalia kuomba kujiunga na Jumuiya hiyo, miaka 10 iliyopita, na mazungumzo na mashauriano kuhusu ombi hilo yataendelea hadi Septemba tarehe 5.

Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa ni kuangalia iwapo sheria ya Somalia, zinaendana na mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku Katibu Mkuu wa EAC Peter Mathuki akisema, ana matumaini kuwa Somalia itafanikiwa.

Suala la usalama linapewa nafasi kubwa kwenye mazungumzo hayo, kutokana na Somalia kukumbwa na changamoto ya kundi la Al Shabab.

Somalia, ina urefu wa Kilomita Elfu 3 wa eneo la Bahari Hindi, inayounganisha na Bahari Nyekundi, na iwapo itafanikiwa kuingia EAC, itapanua fursa za biashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.