Pata taarifa kuu

Niger: Maelfu ya wafuasi wa utawaa wa kijeshi wakusanyika Niamey na Agadez

Maelfu ya watu wameandamana siku ya Jumapili katika miji mikubwa miwili chini Niger kuonyesha uungaji mkono wao kwa utawala wa kijeshi na kuyakosoa madola ya Magharibi, hususan Ufaransa lakini pia Marekani. Maandamano hayo yalikuja siku moja baada ya hotuba ya televisheni ya kiongozi mpya wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, ambapo aliahidi kipindi cha mpito cha miaka mitatu.

Maelfu ya wafuasi wa utawala wa kijeshi waliingia mitaani huko Niamey mnamo Agosti 20, 2023, kudai kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa, ili kurejesha uhuru wao na kuunga mkono Urusi, India na China.
Maelfu ya wafuasi wa utawala wa kijeshi waliingia mitaani huko Niamey mnamo Agosti 20, 2023, kudai kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa, ili kurejesha uhuru wao na kuunga mkono Urusi, India na China. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Ufaransa tulia", "hatutaki vikwazo", ECOWAS "sitisheni uingiliaji kijeshi" ... Haya ni baadhi ya maeneo yaliyotolewa siku ya Jumapili na waandamanaji waliokusanyika kwenye eneo la Place de la Concertation huko Niamey. Walipeperusha bendera za Urusi na Niger, wengine pia walikuwa na bendera za China na India.

Ujumbe wao: kwamba Ufaransa iondoke Niger. Ibrahim Namaiwa ni mmoja wa waandaji wa mkutano huo wa Jumapili. "Tumeweka vipaumbele: kwanza Wafaransa waondoke na kisha tutachunguza hali ya vikosi vingine vya kigeni. Kwa sababu kinachotuvutia sisi ni uhuru kamili wa raia. Tutafanya hatua kwa hatua kujaribu kurudisha kile ambacho kimetwaliwa kutoka kwetu kwa miaka mingi kupitia uvamizi wa nchi yetu na askari wa kigeni. "

Na leo, sio Ufaransa pekee, ambayo inanyooshewa kidole. Marekani nayo sasa hivi. Huko Agadez, katikati mwa nchi, mamia ya watu walikusanyika karibu na uwanja wa ndege ambapo kunapatikana kambi kubwa ya wanajeshi wa Marekani, wakitaka kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani.

Washington ina kikosi cha wanajeshi 1,300 nchini Niger, na kambi yake ya kijeshi huko Agadez ni mojawapo ya kambi kubwa zaidi katika bara la Afrika. Kwa sasa, Pentagon imetangaza udumishaji wa wanajeshi wake nchini Niger, muhimu kwa kupigana dhidi ya makundi ya kijihadi katika eneo hilo, kulingana an Pentagon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.