Pata taarifa kuu

Mafuriko yauwa watu 27 nchini Niger

Nairobi – Mamlaka nchini Niger inasema watu 27 wameripotiwa kuawaua katika mafuriko nchini Niger yaliosabishwa na mvua kubwa inayoshuhudiwa nchini humo tangu mwezi Julai wakati wengine zaidi ya elfu sabini wakiwa wameathirika.

Mikoa ya Maradi, Zinder na Tahoua iliathirika zaidi na nyumba 6,530 zimeanguka, kwa mujibu wa mamlaka nchini humo
Mikoa ya Maradi, Zinder na Tahoua iliathirika zaidi na nyumba 6,530 zimeanguka, kwa mujibu wa mamlaka nchini humo © USAID/FFP
Matangazo ya kibiashara

Msimu wa mvua kati ya mwezi Juni na Septemba mara nyingi husababisha mafuriko mabaya katika taifa hilo linalopâtikana katika eneo lenye jangwa la Afrika Magharibi sawa na maeneo mengine kame ya kaskazini.

Kufikia Agosti 18, mafuriko yamesababisha vifo vya watu 27, kujeruhi watu 30 na kuathiri 71,136, wizara ya masuala ya kibinadamu imesema.

Mikoa ya Maradi, Zinder na Tahoua iliathirika zaidi na nyumba 6,530 zimeanguka, kulingana na wizara hiyo.

Mji mkuu wa Niamey, wenye makazi ya watu milioni mbili, hukabiliwa na mafuriko mara kwa mara ila kwa sasa hayajashuhudiwa.

Msimu wa mvua wa mwaka jana ulisababisha vifo vya watu 195 na kuathiri watu 400,000.

Huduma za hali ya hewa nchini Niger zinasema mvua hiyo inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yameikumba nchi hiyo kwa miaka kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.