Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Niger yakabiliwa na ongezeko la mashambulizi ya wanajihadi na hatari ya kusambaa nchi nzima

Zaidi ya wiki tatu baada ya mapinduzi, wengi wanahofia kuongezeka kwa ukosefu wa usalama nchini Niger, hasa magharibi mwa nchi hiyo, hasa katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu". Kulingana na vyanzo kadhaa, takriban raia 28 waliuawa katika mkoa huu kati ya Jumanne na Jumatano Agosti 16. Wakati huo huo, mashambulizi mawili ya kigaidi yaliua karibu askari na raia zaidi ya ishirini.

Wanajeshi wa Niger wakipiga doria karibu na mji wa Diffa.
Wanajeshi wa Niger wakipiga doria karibu na mji wa Diffa. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Kwa ujumla, mashambulizi tisa ya wanajihadi yamerekodiwa tangu mapinduzi ya Niger mwishoni mwa mwezi Julai. Hali inaowatia wasiwasi waangalizi. Kwa kuongezeka tena kwa mashambulizi ya wanajihadi, duru rasmi zinasema zinahofia "kuzorota kwa kasi kwa hali nchini Niger na huenda hali ya ukosefu wa usalama ikaenea nchi nzima na katika nchi jirani", kwanza kwa sababu Paris imesimamisha ushirikiano wake wa kijeshi na Niger.

Kwa hiyo jeshi la taifa halinufaiki tena na msaada wa jeshi la Ufaransa. Hakuna tena operesheni za pamoja, ndege za kijeshi na ndege zisizo na rubani hazitoi msaada tena na magaidi wanachukua fursa ya ombwe hili.

Kisha, vitisho vya ECOWAS kjingilia kijeshi nchini Niger vilisababisha kupunguzwa kwa idadi ya kijeshi magharibi mwa nchi. Vikosi kutoka Diffa, Dosso na jimbo la Tillabéri vimepelekwa katika mji mkuu wa Niger, Niamey.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.