Pata taarifa kuu
MSAKO-USALAMA

Niger: Nyumba za watu walio karibu na rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum zafanyiwa upekuzi

Vikosi vya usalama na ulii vimefanya msako wa kushtkiza kwenye nyumba za watu walio karibu na Rais Mohamed Bazoum, ambao bado wanazuiliwa na jeshi tangu mapinduzi ya Julai 26, na pia katika nyumba za wmaafisa wa serikali yake na wanachama wa chama chake. Msako huo ulifanyika usiku wa Alhamisi Agosti 17 kuamkia Ijumaa 18, 2023. 

Mji kuu wa Niger, Niamey, Julai 28, 2023.
Mji kuu wa Niger, Niamey, Julai 28, 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Agosti 17 kuamkia 18 huko Niamey, nyumba za maafisa kadhaa wa utawala wa rais wa Niger, Mohamed Bazoum, "zilifanyiwa msako" na watu, ambao baadhi yao walikuwa na silaha.

Katika tukio hili, kulingana na mashahidi, pesa na vitu vya thamani vilikamatwa.

Timu hiyo, iliyo kuwa inaundwa na wanajeshi na angalau raia mmoja, ilitua usiku kkatika nyumba ya Waziri Mkuu wa Rais Mohamed Bazoum, Ouhoumoudou Mahamadou.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, kwa ujumla, nyumba zisizopungua tisa za wajumbe wa serikali ya rais Bazoum na wasaidizi wake zilivamiwa jana usiku, kama ile ya Waziri wa Mambo ya Nje, Hassoumi Massaoudou, nyumba za wabunge Kalla Moutari na Kalla Ankourao, mtawalia Makamu wa Kwanza wa spika wa Bunge la kitaifa na kiongozi mkuu wa PNDS (chama cha Mohamed Bazoum). Lakini pia nyumba za wasaidizi wa mkuu wa nchi aliyepinduliwa: Foumakoye Gado, mwakilishi wake mkuu, Issa Galmai na Daouda Takoubakoye, mtawaliwa mkurugenzi katika ofisi ya rais na naibu mkurugenzi wa ofisi ya rais, na vile vile nyumba ya mlinzi wa rais.

Katika maeneo haya yote, msako ulifanyika. Nyaraka na hasa mali zilichukuliwa. Kwa mujibu wa mashahidi, askari hao walichukua walichoweza kupata: simu, saa na vito, copmyuta, pesa - hadi faranga za CFA milioni 60, au karibu euro 90,000, kutoka kwa nyumba ya Waziri Mkuu - pamoja na magari mawili ya Jenerali Mahamadou Abou Tarka , rais wa Mamlaka ya Juu kwa ajili ya uimarishaji wa amani, ambaye nyumba yake pia ilifanyiwa msako.

Kikihojiwa na RFI, chanzo kilicho karibu na mahakama ya Niger kinadai kutofahamu misako hii. Chanzo iki kinaongeza kuwa Niger kwa sasa inatawaliwa na utawala wa kipekee ambapo sheria haziheshimishwi .

Mmoja wa watu ambao nyumba yzao zilifanyiwa msako anasikitika kwa kutoona hati ya upekuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.