Pata taarifa kuu

Marekani yamteua rasmi balozi mpya nchini Niger licha ya mapinduzi

Balozi mpya wa Marekani hivi karibuni atatua Niger kushiriki katika juhudi za kidiplomasia zinazolenga kurejesha serikali halali, iliyopinduliwa na wanajeshi, Washington imesema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken. REUTERS - LEAH MILLIS
Matangazo ya kibiashara

Mwanadiplomasia Kathleen FitzGibbon aliidhinishwa na Bunge la Seneti mnamo Julai 27, siku moja baada ya jeshi kuchukua mamlaka. Alikuwa akisubiri kurasimishwa kwa uteuzi wake kwa karibu mwaka mmoja, kutokana na vita vya kisiasa vilivyomlenga yeye mwenyewe.

"Tunafanya kinachowezekana ili Balozi FitzGibbon awasili katika mji mkuu wa Niger, Niamey," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Vedant Patel amewaambia waandishi wa habari.

Amehakikisha kwamba kuwasili huku hakumaanishi kwamba Marekani inaidhinisha mapinduzi ya kijeshi na kwamba Washington bado inataka kuachiliwa huru na kurejea madarakani kwa rais mteule Mohamed Bazoum.

"Hii si ishara ya mabadiliko katika sera ya Marekani, lakini kuhusika kwake kunaendelea" katika mgogoro huu, amesema.

Bi FitzGibbon, ambaye ana tajriba kubwa barani Afrika, atahamia Niamey licha ya kuondoka mapema mwezi Agosti kwa wafanyakazi wa ubalozi wasiokuwa wa lazima.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inafuatilia kwa karibu hali nchini Niger. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amezungumza mara kadhaa na Rais Bazoum na maafisa wa eneo hilo, na naibu wake wa pili, Victoria Nuland, alifanya ziara ya kushtukiza mjini Niamey wiki iliyopita ili kukutana na viongozi wa mapinduzi.

Nchini Niger kuna wanajeshi wa Marekani na Ufaransa wanaoendesha operesheni dhidi ya makundi ya wanajihadi wanaoendesha ukatili wao katika ukanda wa Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.