Pata taarifa kuu

Niger: Rais Bazoum anayezuiliwa nyumbani kwake 'atembelewa na daktari wake'

Rais wa Niger Mohamed Bazoum, aliyetekwa katika makazi yake ya rais huko Niamey tangu mapinduzi yaliyompindua Julai 26, "ametembelewa na daktari wake" siku ya Jumamosi, mmoja wa washirika wake wa karibu ameliambia shirika la habari la AFP.

Mwanamke aliyeshikilia picha ya Rais aliyepinduliwa wa Niger Mohamed Bazoum, 63, anayezuiliwa na wanajeshi pamoja na familia yake katika makazi yake rasmi huko Niamey tangu Julai 26, wakati wa maandamano nje ya ubalozi wa Niger huko Paris mnamo Agosti 5, 2023.
Mwanamke aliyeshikilia picha ya Rais aliyepinduliwa wa Niger Mohamed Bazoum, 63, anayezuiliwa na wanajeshi pamoja na familia yake katika makazi yake rasmi huko Niamey tangu Julai 26, wakati wa maandamano nje ya ubalozi wa Niger huko Paris mnamo Agosti 5, 2023. AFP - STEFANO RELLANDINI
Matangazo ya kibiashara

"Rais wa Jamhuri", Mohamed Bazoum, "ametembelewa na daktari wake leo", ambaye "pia alimletea chakula", pamoja na mwanawe na mkewe wanaozuiliwa pamoja naye, mmoja wa washirika wake wa karibu amebainisha.

"Anaendelea vizuri licha ya hali inayomkabili," ameongeza.

Wawakilishi kadhaa wa mashirika na nchi washirika wa Niger kabla ya mapinduzi wameelezea wasiwasi wao kuhusu mazingira ambamo anazuiliwa na hali ya afya ya rais aliyeondolewa madarakani.

Siku ya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, alielezea "wasiwasi wake mkubwa" kuhusu "kuzorota kwa mazingira ambamo anazuiliwa" Bw. Bazoum.

"Matendo kama haya dhidi ya rais aliyechaguliwa kidemokrasia kupitia mchakato wa kawaida wa uchaguzi hayakubaliki," alishutumu.

Umoja wa Ulaya (EU) pia umeonyesha "wasiwasi wake mkubwa", ukitumia maneno sawa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye alisema "amechukizwa" na kukataa kwa viongozi wa kijeshi kumwachilia Mohamed Bazoum.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia alisema "anatiwa wasiwasi" na "hali ya kusikitisha ambayo Rais Bazoum na familia yake wanaeishi," Umojawa Mataifa umesema katika taarifa yake.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch ambalo lilizungumza na Bw. Bazoum, lilielezea jinsi familia yake inavyotendewa kama "kinyama na kikatili".

Ziara ya daktari wa Mohamed Bazoum inakuja siku mbili baada ya kuidhinishwa kwa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kupeleka "kikosi cha dharura" cha jumuiya hiyo kwa nia ya uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.