Pata taarifa kuu

Niger: Jeshi laishutumu Ufaransa kwa kukiuka anga yake na kuwaachilia huru 'magaidi'

Mvutano umeongezea tangu siku ya Jumatano kati ya mamlaka ya kijeshi nchini Niger na Ufaransa, siku moja kabla ya mkutano muhimu wa ECOWAS. Utawala wa kijeshi nchini Niger umeishutumu Ufaransa kwa kukiuka anga ya Niger na kuwaachia huru magaidi. hata hivyo Paris imekanusha madai hayo ikisema hayana msingi wowote. 

Waandamanaji wakipeperusha bendera ya Niger wakati wa maandamano ya Siku ya Uhuru huko Niamey mnamo Agosti 3, 2023.
Waandamanaji wakipeperusha bendera ya Niger wakati wa maandamano ya Siku ya Uhuru huko Niamey mnamo Agosti 3, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Baraza la Ulinzi wa Taifa (CNSP), linaishutumu Ufaransa kwa "kupanga kuhatarisha usalama" kwa lengo la "kudhoofisha CNSP na kuchochea mgawanyiko na raia wa Niger".

Viongozi wa mapinduzi nchini Niger wanatoa mfano wa "wafungwa 16 wa kigaidi walioachiliwa kwa upande mmoja na Ufaransa". Kulingana na utawala wa kijeshi, kisha walikutana kuandaa mashambulizi katika eneo la mipaka mitatu.

Viongozi wa mapinduzi pia wanaishutumu Ufaransa kwa kukiuka anga yake ambayo ilifungwa siku ya Jumapili. Ndege ya jeshi la Ufaransa A-400M iliondoka muda mfupi baada ya saa kumi na mbili Jumatano asubuhi, saa za Niger kutoka Ndjamena. Kulingana na utawala wa kijeshi, mara tu ilipoingia kwenye anga ya Niger bila idhni, ndege hiyo ilikata mawasiliano yote kwa zaidi ya saa nne.

Jaribio la kupotosha ukweli wa mambo

'Madai yasiyo na msingi' yaliyokanushwa vikali na Ufaransa. Katika taarifa yake ya pamoja, Wizara ya Mambo ya Nje na ile ya Ulinzi ya Ufaransa zinaeleza kuwa wanajeshi walioko Niger wapo kwa ajili ya kupambana na makundi ya kigaidi. Na wanakumbusha kwamba hii ilifanyika kwa hatari ya maisha ya askari kadhaa wa Ufaransa.

Kuhusiana na ndee hiyo, Paris pia inakanusha. Ndege hii iliidhinishwa na kuratibiwa na vikosi vya Niger. Uidhinishaji ulitolewa kwa maandishi. Ufaransa inasema, matamshi haya yanajumuisha "jaribio la kupotosha ukweli wa mambo" katika mkesha wa mkutano wa ECOWAS.

Mamlaka ya Niger imeamua kuongeza kiwango cha tahadhari katika nchi nzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.