Pata taarifa kuu

Niger : Ufaransa inaunga mkono suluhu la kidiplomasia

Nairobi – Wiki mbili baada ya mapinduzi nchini Niger, Ufaransa inaonekana kuachana na msimamo wake mkali na sasa inaunga mkono suluhu ya kidiplomasia kutumiwa. 

 Paris imeendelea kusisitiza kuwa inaunga mkono harakati wa kurejesha demokrasia katika taifa hilo la Afrika Magharibi
Paris imeendelea kusisitiza kuwa inaunga mkono harakati wa kurejesha demokrasia katika taifa hilo la Afrika Magharibi REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Watalaam wanasema kauli ya Jumanne ya Ufaransa kuunga mkono mchakato wa kidiplomasia unaonesha kuwa, mpango wa kutumia jeshi kumrejesha rais Mohammed Bazoum madarakani, unaonekana kusitishwa kwa sasa. 

Hata hivyo, Paris imeendelea kusisitiza kuwa inaunga mkono harakati wa kurejesha demokrasia katika taifa hilo la Afrika Magharibi,  huku ikiachia jukumu hilo nchi za ECOWAS,hii ni kwa mujibu wa afisa wa Wizara ya Mambo ya nje. 

Awali, Ufaransa ilikuwa imetangaza kuunga mkono Jumuiya ya ECOWAS ambayo ilikuwa imepanga kutuma jeshi nchini Niger, iwapo uongozi wa kijeshi usingerudisha uongozi wa kiraia kufikia Jumapili iliyopita. 

Wiki iliyopita ujumbe wa ECOWAS haukufanikiwa kukutana na uongozi wa jeshi ambao umesema kwa sasa hauwezi kukutana na wawakilishi hao wa nchi za Afrika Magharibi kwa sababu za kiusalama. 

Mwanadiplomasia wa Marekani, Victoria Nuland naye wiki hii amekutana na wakuu wa jeshi jijini Niamey, na kukiri kuwa mazungumzo yalikuwa magumu. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.