Pata taarifa kuu

Niger: Urusi yataka 'mazungumzo' ili kuepusha 'kuzorota kwa hali ya usalama'

Urusi imetoa wito Jumatano kwa "mazungumzo" ili kuepusha "kuzorota kwa hali" nchini Niger, nchi ya Saheli iliyovurugwa na mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita, ikionya dhidi ya uingiliaji wowote wa kijeshi kutoka nje ya nchi.

Wananchi wa Niger wanashiriki maandamano yaliyoitishwa na wafuasi wa kiongozi wa mapinduzi Jenerali Abdourahmane Tchiani mjini Niamey, Niger, Jumapili, Julai 30, 2023. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema Jumanne, Agosti 1, 2023 Ufaransa inapanga kuwahamisha watu wanaotaka kuondoka Niger baada ya mapinduzi wiki iliyopita katika koloni hilo la zamani la Ufaransa.
Wananchi wa Niger wanashiriki maandamano yaliyoitishwa na wafuasi wa kiongozi wa mapinduzi Jenerali Abdourahmane Tchiani mjini Niamey, Niger, Jumapili, Julai 30, 2023. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema Jumanne, Agosti 1, 2023 Ufaransa inapanga kuwahamisha watu wanaotaka kuondoka Niger baada ya mapinduzi wiki iliyopita katika koloni hilo la zamani la Ufaransa. AP - Sam Mednick
Matangazo ya kibiashara

"Tunaona kuwa ni muhimu sana kutoruhusu kuzorota zaidi kwa hali nchini Niger, tunaamini kwamba ni muhimu kuandaa mazungumzo ya kitaifa ili kurejesha amani ya kiraia, kuhakikisha sheria na utulivu," kulingana na mashirika ya habari ya Urusi yakimnukuu msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova amesema.

Italia yawahamisha raia 68 wa kigeni

Takriban raia 70 wa kigeni wanaoishi nchini Niger waliwasili Roma Jumatano asubuhi, wakihamishwa na Italia kwa sababu za usalama baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea wiki iliyopita katika nchi hii ya Sahel, mamlaka ya Italia imesema.

Ndege ya Jeshi la Wanahewa la Italia Boeing 767 ambayo iliondoka Niamey, ilitua muda mfupi baada ya saa kumi na moja alfajiri kwenye uwanja wa ndege wa Ciampino huko Roma ikiwa na raia 99 wa Italia na mataifa mengine.

Wizara ya Mambo ya Nje, kwa upande wake, ililiambia shirika la habari la AFP kuwa kati ya raia 68 waliohamishwa (kwa ombi lao) ni Waitaliano 36 na Wamarekani 21. Wanajeshi kumi na nane wa Italia pia walirejeshwa nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.