Pata taarifa kuu

Niger: Ubalozi wa Ufaransa walengwa na waandamanaji, Paris yajibu

Ili kuonyesha uungwaji wao mkono  kwa utawala wa kijeshi na mapinduzi yaliyopelekea kuondolewa madarakani kwa Mohamed Bazoum, maelfu ya wananchi wa Niger wameingia mitaani katika mji mkuu wa Niger,  Niamey, Jumapili hii asubuhi.

Waandamanaji wakiwa wameshikilia bango kutoka Ubalozi wa Ufaransa mjini Niamey, Julai 30, 2023.
Waandamanaji wakiwa wameshikilia bango kutoka Ubalozi wa Ufaransa mjini Niamey, Julai 30, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika karibu saa 9 asubuhi kwa saa za Niger Jumapili Julai 30 mbele ya makao makuu ya Bunge la kitaifa la Niger kwenye eneo la Place de la Concertation, eneo kubwa zaidi la Niamey, kuunga mkono viongozi wa kijeshi. Mkutano wa waandamanaji hatimaye ulirushwa moja kwa moja kwenye redio na televisheni vya taifa (RTN), wakati ambapo wazungumzaji wamekaribisha hatua ya viongozi wa mapinduzi nchini Mali na Burkina Faso na kutoa maneneo ya chuki dhidi ya Ufaransa na ECOWAS, wakati jumuiy hiyo ya kikanda ilikuwa ikikutana nchini Nigeria kutathmini hali nchini humo. Bendera chache za Urusi zilionekana wakati wa mkutano huo.

Mara baada ya mkutano kumalizika, waandamanaji walijaribu kukusanyika kwenye ikulu ya rais, ambapo Mohamed Bazoum bado anazuiliwa tangu Jumatano. Lakini walizuiliwa karibu na randabauti na idadi kikubwa ya wanajeshi, ambao waliwazuia kuendelea na maandamano yao kuelekea ofisi ya rais. Baadhi ya waandamanaji walichagua kuelekea Yantala, eeo ambalo balozi za nchi kadhaa zinapatikana, ikiwa ni pamoja na balozi za Marekani na Ufaransa.

Waandamanaji walifika mwendo wa saa 11 mchana mbele ya Ubalozi wa Ufaransa. Baadhi ya waandamanaji waling'oa bango lililokuwa limeandikwa "Ubalozi wa Ufaransa nchini Niger". Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha baadhi yao wakirusha mawe kuelekea kwenye jengo hilo na kujaribu kuvunja milango na madirisha kabla ya kutawanywa na mabomu ya machozi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ilijibu, baada ya tukio hilo, kwa kulaani "unyanyasaji wowote dhidi ya haki za kidiplomasia, ambayo usalama wake ni jukumu la nchi mwenyeji". "Vikosi vya Niger vina wajibu wa kuhakikisha usalama wa milki zetu za kidiplomasia na kibalozi chini ya Mkataba wa Vienna", na "tunawahimiza kutimiza wajibu huu uliowekwa kwao na sheria za kimataifa", imesisitiza Quai d'Orsay.

Ikulu ya Élysée imesema kuwa Emmanuel Macron "hatavumilia shambulio lolote dhidi ya Ufaransa na maslahi yake" nchini Niger na atajibu "mara moja na bila kuzuiliwa".

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa kwenye televisheni, Jenerali Tchiani amewataka waandamanaji kuwa watulivu, akiwaomba kutoshambulia balozi za kigeni nchini Niger.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.