Pata taarifa kuu

Michezo ya Francophonie: OIF yakanusha kuwepo Kinshasa kwa Louise Mushikiwabo

Wakati vyombo vya habari kadhaa vya DRC vimekuwa vikihakikisha kwa siku kadhaa kwamba Mkuu wa sasa wa OIF hatakiwi na serikali ya Kinshasa, msemaji wa serikali ya Kongo alihakikishia Jumatatu, Julai 24 jioni kwamba Louise Mushikiwabo atakuwepo Kinshasa, kwa ufunguzi wa Michezo ya La Francophonie, akitaja utamaduni wa OIF. Ni uongo mtupu, amekanusha Jumanne, Julai 25 msemaji wa shirika hili ambaye anaeleza kuwaKatibu mkuu wa OIF hatakwenda DRC, akifutilia mbali madai ya upande wa Kongo.

Katibu Mkuu wa OIF, Louise Mushikiwabo. Picha iliyopigwa Januari 7, 2019, Paris.
Katibu Mkuu wa OIF, Louise Mushikiwabo. Picha iliyopigwa Januari 7, 2019, Paris. AFP - LIONEL BONAVENTURE
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Kongo hata hivyo alikuwa wazi jana: "Bi. Louise Mushikiwabo hakika atakuwa Kinshasa" kwa sababu "tukio la Michezo ya Francophone ni tukio la OIF", alielezea, akimaanisha kuwa atahudhuriamichezo hii kama mkuu wa OIF na si mwakilishi wa nchi yake ya asili ya Rwanda, ambayo uhusiano na DRC uko katika hali mbaya. Kinshasa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliishutumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao wamekalia sehemu ya mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Patrick Muyaya alitoa hoja kwa kuhakikisha kuwa itifaki ya matumizi wakati wa hafla ya ufunguzi itahitaji katibu mkuu wa shirika la kimataifa la muungano wa nchi zinazozungumza Kifaransa, La Francophonie. "Kinshasa haiwezi na ubaguzi wa kiwango hiki, kwa sababu ni mila katika ngazi ya OIF", aliongeza Patrick Muyaya.

Lakini sasa, msemaji wa OIF, Oria K. Vande weghe, aliharakisha kukanusha tangazo hili leo, na kuhakikisha kwamba Louise Mushikiwabo hatasafari kwenda Kinshasa.

Sababu ? Anahakikisha kwamba serikali ya Kongo ilikuwa imejitolea kwa hiari yake kwamba Waziri wake wa Mambo ya Nje atampa mwaliko. Lakini mkutano huo "ulikatishwa" bila maelezo yoyote, ameongeza msemaji wa OIF. "Mkanganyiko" ambao ulisababisha, anasema, katibu mkuu, kufuta ushiriki wake na kumkabidhi naibu wake, msimamizi wa OIF Caroline St-Hilaire, ambaye amesawili Kinshasa leo jioni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.