Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Watoto wakabiliwa na hali ngumu nchini Sudan

Mapigano yameendelea Jumatatu nchini Sudan katika siku ya 100 ya vita ambavyo bado vinaonekana kutokuwa na matumaini ya kumalizika, bila mshindi na ambavyo vinaua au kujeruhi mtoto kila baada ya saa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya watu milioni 3.3 wamekimbia makazi yao nchini Sudan.
Zaidi ya watu milioni 3.3 wamekimbia makazi yao nchini Sudan. © (AP Photo)
Matangazo ya kibiashara

Tangu Aprili 15, jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane na wanamgambo wa Jenerali Mohamed Hamdane Daglo wamekuwa wakitoa kauli mara kwa mara kwamba wanataka vita "kushinda au kufa". Takriban watu 3,900 wameuawa, kulingana na ripoti ya kukadiriwa idadi ya vifo, kwani miili inayotapakaa barabarani inakuwa vigumu kuihesabu.

Miongoni mwao ni "angalau watoto 435", huku wengine wasiopungua 2,025 wakijeruhiwa, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF. "Kila siku, watoto wanauawa, kujeruhiwa, kutekwa nyara, na hawana shule, hospitali na miundombinu iliyoharibiwa au kuporwa," limeongeza shirika la Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya watu milioni 3.3 wamekimbia makazi yao nchini Sudan - ikiwa ni pamoja na zaidi ya 700,000 nje ya nchi. Na mamilioni zaidi wanakabiliwa na njaa. Sasa zaidi ya nusu ya Wasudan milioni 48 wanahitaji misaada ya kibinadamu ili kuishi, lakini mashirika yasiyo ya kiserikali na Umoja wa Mataifa wanajitahidi kuwasaidia kutokana na ukosefu wa vibali kutoka kwa mamlaka na ufadhili kutoka kwa wafadhili wa kimataifa.

Siku ya Jumatatu, mamlaka ilitangaza kuwa ilifunga barabara ya mwendokasi inayounganisha Khartoum na Darfur kwa sababu "inatumiwa na waasi kusafirisha bidhaa zilizoporwa kutoka kwa raia na kuleta mamluki nchini Sudan". Jeshi limebaini: "Gari lolote lintakalo safiri kupitia barabara hiyo itachukuliwa kama gari la waasi, litashambuliwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.