Pata taarifa kuu

Kenya na EU zimetiliana saini makubaliano kuhusu mkataba wa kibiashara baiana yao

NAIROBI – Umoja wa Ulaya na nchi ya Kenya zimetiliana  saini makubaliano kuhusu mkataba wa kibiashara baiana yao, hatua inayokuja wakati huu EU ikitafuta uhusiano wa kina wa kiuchumi na Afrika. 

Kenya na Umoja wa Ulaya zimetiliana saini makubaliano kuhusu biashara
Kenya na Umoja wa Ulaya zimetiliana saini makubaliano kuhusu biashara © Hussein Mohamed
Matangazo ya kibiashara

"Leo ni wakati wa kujivunia sana kwa Kenya, ambapo naamini pia ni wakati wa kujivunia sana kwa Umoja wa Ulaya," Waziri wa Biashara wa Kenya Moses Kuria alisema baada ya kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi wa EU na Kenya na Kamishna wa Biashara wa EU Valdis Dombrovskis. 

Mara baada ya kuidhinishwa na kuanza kutumika, mpango huo wa kibiashara unatarajiwa kuipa Kenya kufikia soko la Ulaya ambapo inatuma sehemu kubwa ya mauzo yake nje.

Kenya inatuma bidhaa zake za kilimo kama vile chai na kahawa maarufu nchini humo  na asilimia 70 ya maua yake kwa nchi za kigeni. 

"Hii ni siku muhimu sana kwa uhusiano wa EU na Kenya," Dombrovskis alisema katika hafla iliyohudhuriwa pia na Rais wa Kenya William Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua. 

 "Ninatazamia kusonga mbele haraka iwezekanavyo ili kutia saini na kutekelezwa kwa mafanikio kwa mkataba huu ili watu wetu na uchumi kuanza kuhisi manufaa yake." 

Mkataba huu iliyotia saini Kenya, unafuatia majadiliano ya muda mrefu, ambapo tangu mwaka 2016 nchi wanachama za jumuiya ya Afrika Mashariki zilikataa kutia saini ushirikiano huu kwa kile zilisema utanufaisha zaidi Ulaya kuliko Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.