Pata taarifa kuu

Tunisia: Mpango wa EU na serikali ya Tunis kuhusu wahamiiaji wakosolewa

NAIROBI – Masharika ya kiraia nchini Tunisia yamethumu mpango wa Umoja wa Ulaya na serikali ya Tunisia kutaka kushirikiana kuzuia idadi ya wahamiaji wanaokimbilia ulaya.

Mashirika ya kiraia nchini Tunisia yamekashifu mpango wa serikali nchini humo na EU kuhusu wahamiaji
Mashirika ya kiraia nchini Tunisia yamekashifu mpango wa serikali nchini humo na EU kuhusu wahamiaji AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Masharika hayo yanadai kwamba mpango wa Umoja wa Ulaya kutaka kufufua uchumi wa Tunisia kwa kuipa Dolla billini Moja, huku Tunisia ikitarajiwa kuzuia wahamiaji kukimbilia ulaya, ina maana kuwa Umoja wa Ulaya unaunga mkono utawala dhalimu wa rais Kais saied.

Masharika hayo yameongeza kuwa ahadi ya pesa nyingine dolla millioni 113 ya usimamizi wa maeneo ya mipakani, itawasidia polisi wa Tunisia kuendelea kukiuka haki za raia wa taifa hilo ambao ni wapinzani wa serikali , wakimbizi na wahamiaji .

Aidha mashirika hayo yametuhumu viongozi wa umoja wa Ulaya wakiongozwa na mwenyekiti wa tume hiyo Ursula Von Der Leyen, kwa kukosa kukemea vitendo viovu vinavyotekelezwa na serikali ya Kais Saied, badala yake lengo lao kuu lilikuwa kuzuia wahamiaji wanaotua Italia kupitia Tunisia

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.