Pata taarifa kuu

Sudan yamtangaza mjumbe wa UN, Volker Perthes kama mtu asiyetakiwa

NAIROBI – Serikali ya Sudan imetangaza kuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Volker Perthes, ni mtu asiyetakiwa katika taifa hilo, linaloendelea kushuhudia mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF. 

Volker Perthes, Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan
Volker Perthes, Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa na Wizara ya Mambo ya nje, ambayo katika taarifa yake imesema, imemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress, kumfahamisha uamuzi wa mjumbe wake kutotakiwa nchini humo kuanzia siku ya Alhamisi. 

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah al-Burhan mwezi uliopita, kumtuhumu Perthes kwa kuchochea vita vinavyoendelea na kumtaka Guteress, kumwondoa. 

Wakati wa tangazo hilo, Perthes alikuwa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya mazungumzo ya kidiplomasia. 

Tangu kutumwa kwake nchini Sudan mwaka uliopita, amekuwa akishtumiwa na jeshi pamoja na waandamanaji kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo. 

Hata hivyo, Guteress amekuwa akisema ana imani kubwa na Perthes ambaye wiki iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha azimio la kuongeza Ujumbe wake nchini Sudan kwa miezi sita zaidi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.