Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambakiza mjumbe wake aliyetangazwa kama mtu asiyetakiwa Sudan

Nchini Sudan, vikosi vya jeshi vya Jenerali al-Burhan na vikosi vya kijeshi vya Jenerali Hemedti vimekubali kanuni ya usitishaji vita kwa saa 24, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imetangaza siku ya Ijumaa Juni 9, 2023, nchi ambayo upatanishi unafanyika kuhusu mzozo huu ulioanza tarehe 15 Aprili. Mapema kidogo, serikali ya Sudan ilitangaza mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, raia wa Ujerumani kama mtu asiyetakiwa. Maelezo.

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes akizungumza kufuatia kutiwa saini kwa makubaliano ya awali kati ya viongozi wa kijeshi na raia, yenye lengo la kumaliza mgogoro mkubwa uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka jana, katika mji mkuu Khartoum mnamo Desemba 5, 2022.
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes akizungumza kufuatia kutiwa saini kwa makubaliano ya awali kati ya viongozi wa kijeshi na raia, yenye lengo la kumaliza mgogoro mkubwa uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka jana, katika mji mkuu Khartoum mnamo Desemba 5, 2022. AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, alitangazwa kama mtu asiyetakiwa na serikali ya Sudan, ambayo inamtuhumu kuhusika katika vita. Hii si mara ya kwanza kwa utawala wa kijshi kumshambulia mjumbe wa Umoja wa Mataifa.

Kwa uamuzi huu, serikali ya Sudan inajibu moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye aliamua kumbakiza Volker Perthes kwenye wadhifa wake. Hata hivyo, Jenerali al-Burhan alieomba abadilishwe katika barua aliyomuandikia António Guterres binafsi.

Uteuzi wa serikali ya Sudan wa mjumbe wa Umoja wa Mataifa "kama mtu asiyetakiwa" ni "kinyume" na kanuni za Umoja wa Mataifa na "hautumiki", msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema siku ya Ijumaa, akibainisha kuwa hadhi ya Volker Perthes "haijabadilika".

Kwa waangalizi kadhaa wanasema, jeshi la Sudan linataka kudhoofisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa ili kusalia madarakani na kuepuka haki. Itakumbukwa kwamba wanashutumiwa kwa uhalifu wa kivita huko Darfur na, kulingana na wachambuzi hawa, wanashikilia nyadhifa zao ili wasihukumiwe.

Hata hivyo, tangu kuwasili kwake, kufuatia makubaliano ya amani ya Juba ya mwaka 2020, mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa alifanya kazi ya kuwakumbusha wanajeshi kuhusu haja ya kuanzisha tena mchakato wa mazungumzo ya kisiasa na waliotia saini makubaliano hayo, pamoja na wale ambao hawakutia saini.

'Volker Perthes ana mtazamo wa kweli wa Sudan'

Wakati wowote wanajeshi wanapokuwa chini ya shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kurudisha mamlaka kwa raia, wamekuwa wakishambulia ujumbe wa Umoja wa Mataifa. Kisha walianza kukuchukuwa uamuzi wa kutotoa tena visa kwa maafisa wake.

Kazi ya misheni sasa ni ngumu zaidi, hasa kwani Volker Perthes atalazimika kufanya kazi kutoka Nairobi.

Gérard Prunier, mtaalamu katika Afrika Mashariki, pia anasisitiza kuhusu Volker Perthes: “Mtu huyu ana mtazamo wa kweli kupita kiasi kuhusu Sudan. Yeye hamuungi mkono Burhan wala Hemedti. Lakini angependa kuona uhasama ulioanza Aprili 15 ukikoma. "Na mtafiti anahitimisha akisema: "Matokeo, kwa maoni yangu, hayatakuwa mengi. Kwa sababu hivi sasa Umoja wa Mataifa, kisiasa, ni kama maiti. Hawawezi kufanya lolote tena. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.