Pata taarifa kuu

Idadi ya wahamiaji inaongezeka kwa kasi nchini Niger, kulingana na IOM

Mamia ya watu walikufa au kutoweka kwenye njia zisizo halali wanazotumia wahamiaji kwa kuvuka kutoka Niger hadi Afrika Kaskazini, kupitia jangwani, katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu. Hili ndilo linalojitokeza kutokana na ripoti ya wimbi la idadi ya watu nchini Niger, iliyochapishwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), kupitia Mfumo wake wa Kufuatilia watu wanaohama kutoka eneo moja kwenda lingine.

Raia wa Niger na wahamiaji wa mataifa mengine wanaondoka kuelekea Libya Juni 4, 2018.
Raia wa Niger na wahamiaji wa mataifa mengine wanaondoka kuelekea Libya Juni 4, 2018. AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu nchini Niger imeongezeka kwa 20% katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ikilinganishwa na miezi mitatu iliyopita ya mwaka 2022, inabainisha ripoti hii ya IOM. Theluthi moja ya idadi hii wanabaki nchini Niger, wale wanaosalia huvuka mpaka, iwe ni kuingia au kutoka nchini humo. Data inakusanywa kutoka kwa wasafiri katika sehemu kumi za kuvukia ili kuchanganua mienendo ya uhamaji huu.

Ongezeko hili, kwa mujibu wa ripoti hii, linaelezewa na watu waliohamishwa kuelekea maeneo ya dhahabu na kufukuzwa kwa wahamiaji kutoka Algeria na Libya.

Idadi kubwa ya watu walioangaliwa na timu za IOM kati ya mwezi Januari na mwezi Machi ni wanaume watu wazima. 18% ni wanawake, 9% ni watoto wadogo ambao wanatoka hasa nchini Niger au nchi jirani, na hasa wakitoa sababu za kiuchumi za kuhama kwao.

Harakati hizi zinafanywa chini ya hali ngumu kwa wale wanaotumia njia zisizo halali kwa kuvuka kutoka Niger kuelekea Afrika Kaskazini na kisha Ulaya. Watu 528 walikufa au kutoweka katika kipindi kama hicho, nchini Niger, Algeria na Libya kutokana na usafiri hatari, magonjwa, vurugu au njaa, upungufu wa maji mwilini au ukosefu wa makazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.