Pata taarifa kuu

Niger: Wahamiaji waishi katika mazingira magumu Assamaka

Kila wiki, mamia ya wahamiaji wanaorudishwa kutoka Algeria wanakwama katika kijiji cha Assamaka, kijiji cha kwanza kwenye mpaka wa Niger. Sasa wako zaidi ya 4,500 wanaotangatanga katika kisiwa hiki kidogo cha nchi kavu chenye wakaazi wenye maisha duni.

Baada ya kufukuzwa na kutembea kilomita 15 jangwani, sasa wanajikuta katika kijiji hiki ambacho wanakichukulia kuwa na ni taifa jipya.
Baada ya kufukuzwa na kutembea kilomita 15 jangwani, sasa wanajikuta katika kijiji hiki ambacho wanakichukulia kuwa na ni taifa jipya. © 2020 IOM Niger
Matangazo ya kibiashara

Waguine, Wa Ivory Coast, Wasyria, Wabangladeshi, ni miongoni mwa wahamiaji hao waliofukuzwa nchini Algeria na wanaishi katika mazingira magumu huko Assamaka. Baada ya kufukuzwa na kutembea kilomita 15 jangwani, sasa wanajikuta katika kijiji hiki ambacho wanakichukulia kuwa na ni taifa jipya.

Kituo cha usafiri kinachosimamiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), shirika kuu la kiserikali katika nyanja hii, kimezidiwa na wingi wa watu na kinatunza karibu theluthi moja ya wale wanaorudishwa nyuma. "Tulipowasili hapa, tuliambiwa kwamba hatukutambulika kama wahamiaji wa IOM na hivyo basi, tunapaswa kulipia tu usafiri wetu ili kurejea nchini," amesema Abdoul Karim Bambara, raia wa Côte d'Ivoire.

Huko Assamaka, kunaripotiwa uhaba wa maji, wanapata chakula kisichotosha na wanalala katika mazingira magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.