Pata taarifa kuu

Rais Tshisekedi ahitimisha ziara yake ya kikazi nchini China

NAIROBI – Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, amemaliza ziara ya siku nne nchini China, alikotia saini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kibiashara na uchumi na mwenyeji wake, XI Jinping.

Felix Tshisekedi wa DRC amekuwa ziarani nchini China ambapo alikutana na mwenyeji wake Xi Jinping
Felix Tshisekedi wa DRC amekuwa ziarani nchini China ambapo alikutana na mwenyeji wake Xi Jinping AP - Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili, wameapa kuimarisha zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili, hasa kwenye maeneo ya kimkamati hasa uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Ushikiano zaidi unatarajiwa kushuhudiwa kwenye sekta ya teknolojia, Kilimo, mazingira na elimu.

Kuhusu ushirikiano katika sekta ya madini, macho ni kuhusu namna mataifa hayo mawili sasa yatashirikiana kuhusu mikataba iliyotiwa saini mwaka 2007 ambapo kampuni kutoka China, zinatakiwa kuwekeza lakini makubaliano hayo yajatekelezwa kikamilifu.

Akiwa nchini China, rais Tshisekedi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu kuyanufaisha kwa usawa mataifa hayo mawili, huku China ikitumai kuwa Kinshasa itahakikisha mazingira ya uwekezaji yanaimarishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.