Pata taarifa kuu

Mamia ya raia wajitokeza kwa maandamano nchini Libya

Nairobi – Mamia ya Raia nchini Libya wamejitokeza barabarani kwa mandamano dhidi ya Jeshi kwa tuhuma za kuwasajili wahamiaji na kuitaka serikali kudumisha haki.

Raia wa Libya waandamana kulitaka jeshi kusitisha  usajili wa wahamiaji
Raia wa Libya waandamana kulitaka jeshi kusitisha usajili wa wahamiaji Reuters/Benoît Tessier
Matangazo ya kibiashara

Raia kwenye eneo la magharibi  katika mji wa Zawiya waliandamana hapo jana kulishinikiza jeshi kuacha kuwasajili wahamiaji wanaoshukiwa kuhusika katika vitendo vya unyanyasaji .

Zawiya iko kilomita 45 magharibi mwa mji mkuu wa Tripoli na ni sehemu muhimu yakuondokea kwa wahamiaji wanaotaka kuvuka bahari ya Mediterania kuelekea Ulaya,na wengi hutafuta kazi huko huku wakisubiri kuvuka bahari.

Ghasia zimeshudiwa nchini humo kwa takribani muongo mmoja sasa  tangu kuawawa kwa dikteta Moamer Khadhafi mwaka 2011.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakishtumu mara kwa mara mamlaka na makundi yenye silaha yanayofanya kazi chini ya mwamvuli wa serikali kwa mateso na visa vya unyanyasaji .

Siku chache zilizopita video ilisambaa mtandaoni na kuonyesha baadhi ya raia  wa Libya wakipigwa .Raia waliondamana  wametaka wanajeshi wanaowasajili wahamiaji kuhamishwa kutoka kwa mji huo.

Kufikia sasa hakuna taarifa yoyote kutoka kwa viongozi wa nchi hiyo wala serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.