Pata taarifa kuu

Vifo kutokana na Marburg, nchini Guinea ya Ikweta vyafikia 12

NAIROBI – Wizara ya afya nchini Guinea ya Ikweta, imesema idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko wa virusi vya Marburg imeongezeka hadi 12.

Mtazamo wa chembe za virusi vya Marburg chini ya darubini ya elektroni;
Mtazamo wa chembe za virusi vya Marburg chini ya darubini ya elektroni; Centers for Disease Control and Prevention
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizo ni za awali, kutokana na uchunguzi wa mahabara kufikia Aprili 21, wizara hiyo ikiongeza kuwa watu 116, kwa sasa wanaendelea kuchunguzwa kutokana na hofu ya kutangamana na walioambukizwa.

Kifo cha kwanza kiliripotiwa mnamo Januari 7, katika mkoa wa Kie-Ntem, kabla ya kusambaa hadi jiji la kibiashara la nchi hiyo, Bata.

Virusi  vya Marburg ambavyo vina dalili karibia na vile vya Ebola, husababisha kutokwa na damu na kufeli kwa viungo vya ndani vya mwili, na kifo cha hivi punde kiliripotiwa Aprili, 11, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Guinea ya Ikweta.

Mwezi Machi mwaka huu, Shirika la afya Dunia, WHO, liliomba nchi hiyo kuripoti matukio yoyote kwa shirika hilo, WHO, ikihofu kuwa kuenea kwa magonjwa ya kuambukizana yanaweza kuchipuka na kuathiri mataifa jirani ya Gabon na Cameroon.

Kwa mujibu wa WHO, kasi ya vifo ni kutoka asilimia 24 hadi asilimia 88, katika milipuko ya hapo awali, huku aina ya kirusi na uthibiti wa maambukizo yakizingatiwa.

Kwa sasa wanasayansi hawajafanikiwa kupata chanjo lakini matibabu yanayowezekana ikiwa ni pamoja na bidhaa za damu, matibabu ya kinga na matibabu ya dawa, pamoja na chanjo za mapema za muathiriwa, zinatathminiwa.

Virusi hivi vinachukua jina kutoka kwa mji wa Ujerumani, Marburg, mahali ambapo iligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1967, katika mahabara ambapo wafanyakazi walikuwa wametangamana na nyani wa kijani aliyekuwa ameambukizwa, aliyesafirishwa kutoka nchini Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.