Pata taarifa kuu

Chad: Miaka miwili baada ya kifo cha rais Idriss Déby ukweli hujajulikana kuhusu kifo chake

Miaka miwili iliyopita, Rais wa Chad Idriss Déby aliuawa katika mapigano na waasi wa FACT katika eneo la Kanem, kilomita 300 kaskazini magharibi mwa Ndjamena. Bado ukweli haujulikani kuhusu mazingira halisi ya kifo chake na kuhusu uchunguzi uliofuata.

Wanajeshi wakiandamana wakati wa mazishi ya kitaifa ya Rais wa Chad Idriss Déby Itno huko Ndjamena, Aprili 23, 2021.
Wanajeshi wakiandamana wakati wa mazishi ya kitaifa ya Rais wa Chad Idriss Déby Itno huko Ndjamena, Aprili 23, 2021. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi ulioahidiwa wakati huo juu ya kifo cha Idriss Déby haukuwahi kutoa hitimisho rasmi na la umma, ingawa wapiganaji 455 wa FACT walihukumiwa kifungo cha maisha mnamo Machi 21 kwa, hasa, "ugaidi" na " kuhatarisha usalama  wa rais”. Miongoni mwao, 380 walisamehewa na rais wa mpito na kuachiliwa mnamo Aprili 5. Wengine 55 waliohukumiwa bila kuwepo mahakamani, akiwemo kiongozi wa kundi hilo, Mahamat Mahdi Ali, hawakunufaika na msamaha huo.

Ni nini hasa kilichosemwa wakati wa kesi ya wafungwa wa FACT, ambayo ilisikilizwa katikati ya jangwa katika eneo ambalo Wachad wanaita gereza la Koro Toro? Je, majaji walitaja mazingira ambayo Idriss Déby aliuawa wakati wa mashambulizi ya kundi la waasi? Ni vigumu kujua: mawakili wa utetezi na vyombo vya habari huru havikuweza kufuatilia kesi hiyo.

Ushahidi wa uchunguzi uliwekwa siri

Kwa mujibu wa habari zetu, majaji walikuwa na mahitimisho ya upelelezi, lakini "hawakutaka kuweka mambo haya hadharani wakati wa kesi, ili kulinda heshima ya rais aliyefariki," chanzo cha kiserikali kinafahamu vizuri kesi hii, kimesema.

Kwani uchunguzi "ulifanyika" chanzo hiki kimeongeza. “Watu wote waliokuwa karibu na marshal alipofariki, wasaidizi wake, daktari wake, familia, askari n.k walisikilizwa na majaji na ushahidi wao uliwekwa kwenye ripoti rasmi, chanzo hiki kinaeleza. Daktari pia alitoa ripoti ya sababu za kifo chake, ambayo inabainisha majeraha aliyopata.

Kwa hivyo, ushahidi uliyowekwa siri, ambao unaonyesha maswali ya sehemu ya raia, wadau wa kisiasa na mashirika ya kiraia, ambao wanaendelea kudai "uchunguzi huru".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.