Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

CAR: Wanajeshi 19 waliotekwa nyara waachiliwa

Shirika la Msalaba Mwekundu na Ilani Nyekundu (ICRC) limetangaza Jumanne kuachiliwa kwa wanajeshi 19 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, waliotekwa nyara Februari 14 na muungano wa makundi ya waasi kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo inakabiliwa navita vya kiraia kwa miaka kadhaa.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) wakionekana wakati wa gwaride la kijeshi lililoandaliwa kusherehekea kumbukumbu ya miaka 64 ya uhuru wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, huko Bangui, Desemba 1, 2022.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) wakionekana wakati wa gwaride la kijeshi lililoandaliwa kusherehekea kumbukumbu ya miaka 64 ya uhuru wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, huko Bangui, Desemba 1, 2022. AFP - BARBARA DEBOUT
Matangazo ya kibiashara

Kati ya wanajeshi 20 waliochukuliwa mateka zaidi ya miezi miwili iliyopita, 19 waliachiliwa na "watawasili Birao (Kaskazini) mwendo wa saa kumi na moja jioni na watakaa huko hadi tutakapopanga kurejea kwao Bangui", Yves Van Loo, naibu mkuuwa ujumbe wa ICRC nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ameliambia shirika la habari la AFP. 

Walikuwa wamechukuliwa mateka na waasi wa Muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko (CPC) baada ya "mapigano makali" ambayo yalisababisha hasara "kubwa" za kijeshi, kulingana na serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.