Pata taarifa kuu

Sahel: Watoto zaidi ya milioni 10 wanahitaji msaada: UN

NAIROBI – Umoja wa Mataifa, unasema watoto zaidi ya milioni 10 kwenye nchi za Burkina Faso, Mali na Niger, wanakabiliwa na hali mbaya na kwamba wanahitaji haraka misaada ya kibinadamu, kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama.

Watoto zaidi ya milioni 10 kwenye nchi za Burkina Faso, Mali na Niger wanahitaji msaada
Watoto zaidi ya milioni 10 kwenye nchi za Burkina Faso, Mali na Niger wanahitaji msaada © PBEAHUNYKGE/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF, idadi hii ni mara mbili ya ile iliyoripotiwa mwaka 2020.

Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Afrika Magharibi, Marie-Pierre Poirier, amesema mamia ya watoto wameendelea kunaswa kwenye mapigano na kuna hofu vurugu hizo kuenea kwenye nchi zaidi za Sahel.

Aidha UNICEF imesema mwaka 2022 ulikuwa hatari zaidi kwa watoto kwenye ukanda wa Sahel, ikizitaka pande zinazopigana kujiepusha na mashambulio yanayowalenga watoto, shule, makazi na hospitali.

UNICEF imesema katika taarifa yake kuwa, imepokea sehemu tu ya fedha zilizoahidiwa mwaka uliopita, huku mwaka huu ikitoa wito wa kusaidia karibu dola wa Marekani, milioni 473.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.