Pata taarifa kuu

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris kuzuru Afrika mwezi huu

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris atafanya ziara kati ya mwishoni mwa mwezi Machi na mapema mwezi Aprili nchini Ghana, Tanzania na Zambia, Ikulu ya White House imetangaza siku ya Jumatatu, kufuatia mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika uliofanyika Washington mwishoni mwa mwaka 2022.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akizungumza katika Mkutano wa Usalama wa Munich huko Munich, kuanzia Feb 17 hadi 18 Februari 2023.
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akizungumza katika Mkutano wa Usalama wa Munich huko Munich, kuanzia Feb 17 hadi 18 Februari 2023. AP - Michael Probst
Matangazo ya kibiashara

Mjini Accra, Dar es Salaam na Lusaka, Bi. Harris anatazamiwa kukutana na marais wa nchi hizo tatu "kujadili vipaumbele vya kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na dhamira yetu ya pamoja ya demokrasia, ukuaji jumuishi na endelevu, usalama wa chakula na vita nchini Ukraine," taarifa hiyo imesema.

Makamu wa rais kutoka chama cha Democratic atakwenda huko baada ya ziara  ya Jill Biden, mke wa rais, katika Pembe ya Afrika mwezi Februari, ambapo alitaja rekodi ya ukame na masuala ya kilimo na chakula. Kamala Harris kwa hivyo lazima, kulingana na White House, afanye kazi ili kusaidia "ustahimilivu na kukabiliana na mgooro wa Tabia nchi" katika eneo hilo.

Ziara hiyo inakuja baada ya mkutano wa kilele wa Afrika mwezi Desemba mjini Washington, ambapo Rais Joe Biden alitoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano mpana na Afrika, na huku Marekani ikitaka kudhihirisha uwepo wao barani humo dhidi ya uwekezaji wa China.

Rais kisha aliahidi kuzuru Kusini mwa Jangwa la Sahara, labda mapema mwaka wa 2023, ambapo itakuwa ziara ya kwanza katika ngazi hii tangu Barack Obama, ambaye alizuru Kenya na Ethiopia mwaka wa 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.