Pata taarifa kuu

Afrika kunufaika na dola Bilioni 55 kutoka Marekani kwa kipindi cha miaka mitatu

Rais Joe Biden anatarajiwa kutangaza kuwa Marekani, itatoa dola za Marekani Bilioni 55 kwa ajili ya bara la Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kushoto na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, kulia, wakikutana na Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na Rais wa Niger Mohamed Bazoum wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Marekani mwaka wa 2022, Jumanne, Desemba. 13, 2022 huko Washington.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kushoto na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, kulia, wakikutana na Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na Rais wa Niger Mohamed Bazoum wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Marekani mwaka wa 2022, Jumanne, Desemba. 13, 2022 huko Washington. AP - Evelyn Hockstein
Matangazo ya kibiashara

Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya nje, amesema msaada wa Marekani, hata hivyo, hauzui mataifa ya Afrika, kushirikiana na mataifa mengine.

Waziri Anthony Blinken amesema alipokutana na Sall kwamba Senegal Macky Sall, ambaye pia ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, wakati wa mkutano wa kilele kati ya Afrika na Marekani huko Washington, amesema serikali ya Marekani inajiandaa kutoa tangazo zito siku ya Ijumaa wakati itakapotangaza kuunga mkono mpango wa kuufanya Umoja wa Afrika kuwa mwanachama wa kudumu wa kundi la mataifa yanayoendelea na yaliyoinukia kiuchumi la G20, hatua iliyopongezwa na rais Sall.

Mapema, waziri Blinken aliyataja masuala muhimu kwenye majadiliano na wakuu hao ambayo ni pamoja na mzozo wa mabadiliko ya tabianchi, ulinzi wa Bonde la Kongo na wasiwasi ulioko kati ya DRC na Rwanda, mashariki mwa taifa hilo, huku akionya kwamba China na Urusi zimekuwa zikilidhoofisha bara hilo kwa kuongeza ushawishi wake.

 Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo akizungumza kwenye mkutano huo, ameyataka mataifa ya Afrika kuacha tabia ya kuomba misaada iwapo, bara la Afrika linataka kuheshimiwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.