Pata taarifa kuu

Côte d'Ivoire itakuwa mwenyeji wa Siku ya Mazingira Duniani mnamo Juni 5

Côte d'Ivoire itakuwa mwenyeji wa Siku ya Mazingira Duniani Juni 5, Waziri wa Mazingira na Maendeleo Endelevu wa Côte d'Ivoire, Jean-Luc Assi, ametangaza siku ya Jumatatu wakati wa sherehe za uzinduzi wa tukio hili mjini Abidjan.

Wanawake hutembea kando ya barabara katika njia panda ya Duekoué, mnamo Oktoba 2020.
Wanawake hutembea kando ya barabara katika njia panda ya Duekoué, mnamo Oktoba 2020. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

"Côte d'Ivoire mwaka huu ni nchi mwenyeji wa Siku ya Mazingira Duniani", inayoandaliwa kila mwaka na Umoja wa Mataifa, waziri amesema. Mada ya toleo hili ni "suluhisho la uchafuzi wa plastiki", "janga ambalo linatishia sisi sote", amesema Bw. Assi. Zaidi ya nchi 150 zitashiriki katika siku hii, kumbukumbu ya miaka hamsini ambayo itaadhimishwa mwaka huu.

Jean-Luc Assi amethibitisha kujitolea kwa nchi ya Côte d'Ivoire ambayao inataka kuwa "kielelezo katika suala la maendeleo endelevu". Côte d'Ivoire imeridhia mkataba wa Tabia nchi wa Paris ambao ulianza kutumika mwaka 2016, ili kuweka wastani wa joto duniani chini ya 2°C.

Serikali ya Côte d'Ivoire pia iliamua Mei 2013 kupiga marufuku uzalishaji, uuzaji, umiliki na matumizi ya mifuko ya plastiki. Lakini kuanza kutekelezwa kwa uamuzi huu mwezi Novemba 2014 kulichochea maandamano ya wafanyabiashara mjini Abidjan na sasa hautumiki sana nchini humo.

Toleo hili linafuatia azimio lililopitishwa mwaka wa 2022 na Baraza la Umoja wa Mataifa la kuanzisha "chombo" cha kisheria "kinachofunga" juu ya uchafuzi wa plastiki, iliyopangwa mwishoni mwa 2024.

Kulingana na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP), tani milioni 400 za plastiki huzalishwa duniani kote kila mwaka, nusu ya ambayo imeundwa kwa matumizi moja. Kati ya tani milioni 19 na 23 za plastiki huishia kwenye maziwa, mito na bahari, amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.