Pata taarifa kuu

Uchumi wa Nigeria, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, umedorora

Mfumuko wa bei wa tarakimu mbili, mishahara duni, fedha taslimu na uhaba wa mafuta: Raia wa Nigeria wanakabiliwa na hali mbaya zaidi ya kiuchumi, siku chache kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Jumamosi katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Wanawake wanauza mboga mboga na vyakula vingine sokoni huko Lagos, Nigeria.
Wanawake wanauza mboga mboga na vyakula vingine sokoni huko Lagos, Nigeria. AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

"Ni vigumu sana kuishi nchini Nigeria, kila hali ya maisha ni ngumu, ni vigumu kuishi",  Rotimi Bankole, 54, anasema huku akikata tamaa kutokana na hali inayojiri nchini Nigeria.

Kama mamilioni ya wananchi wenzake, mkazi huyu wa Lagos, mji mkuu wa kiuchumi, anachanganya kazi kadhaa, rasmi na zisizo rasmi, ili kuweza kumudu maisha ya mkewe na watoto watatu. Kando na majukumu yake kama mkurugenzi wa shule, anasimamia biashara ndogo ya uchapishaji, na ameongeza shughuli mpya kwa siku zake ambazo tayari zina shughuli nyingi: dereva wa teksi.

Kuimarika kwa uchumi wa nchi hii inayoozungumza Kiingereza, nchi yenye wakazi milioni 215, 63% ambao ni maskini, itakuwa moja ya masuala makuu ya uchaguzi, pamoja na ukosefu wa usalama (uasi wa kijihadi, uhalifu, madai ya watu wanaotaka kujitenga).

Mzalishaji mkuu wa mafuta ya gari barani, Nigeria ina maliasili nyingi, hasa katika hidrokaboni. Lakini janga la Uviko-19 na kuzuka kwa vita nchini Ukraine vimesababisha uchumi wake kudoroa, na ambao tayari umeathiriwa na ghasia ambazo zinazoofisha kilimo na biashara katika sehemu kubwa za nchi.

Mfumuko wa bei unakaribia 22%, na sarafu ya kitaifa, naira, inaendelea kupoteza thamani dhidi ya dola ambapo kwa sasa naira 750 inauzwa dola moja , dhidi ya naira 200 mwaka wa 2015.

Katika muktadha huu, ikiongezwa kwa mlipuko wa bei ya petroli, ambayo imeongezeka karibu mara mbili (naira 330 kwa lita dhidi ya 165 miezi michache iliyopita).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.