Pata taarifa kuu

Mauritius iko kwenye tahadhari wakati kimbunga Freddy kikikaribia

Mauritius iko katika hali ya tahadhari siku ya Jumatatu wakati kimbunga kikali cha kitropiki kiitwacho Freddy kikikaribia, na safari za ndege kusitishwa na usafiri wa umma kukatizwa katika kisiwa cha Bahari ya Hindi, mamlaka imesema.

Kimbunga Freddy, ambacho huenda kikasababisha mafuriko katika pwani, kinaweza kupita takriban kilomita 120 kaskazini magharibi mwa Mauritius katika sehemu yake ya karibu mapema jioni.
Kimbunga Freddy, ambacho huenda kikasababisha mafuriko katika pwani, kinaweza kupita takriban kilomita 120 kaskazini magharibi mwa Mauritius katika sehemu yake ya karibu mapema jioni. Sarah Tétaud/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Mauritius (MMS) imetoa onyo la kimbunga cha daraja la 3, ikibaini kwamba upepo unaweza kufikia kilomita 300 kwa saa.

Katika taarifa hii, imebainishwa kuwa Kimbunga Freddy kilikuwa saa 07:00 asubhi (03:00 GMT) kwenye umbali wa kilomita 275 kaskazini-mashariki mwa Mauritius na kwamba kilikuwa kikielekea magharibi-kusini-magharibi kwa kasi ya takriban kilomita 30 kwa saa.

"Katika mwelekeo huu, Kimbunga Freddy kinaendelea kukaribia kwa hatari karibu na Mauritius na ni tishio la moja kwa moja kwa kisiwa hicho", Mamlaka ya Hali ya Hewa imeongeza onyo hili, ikitabiri "hali kuwa mbaya" katikati ya mchana na 'hali ya kimbunga' alaasiri.

Kimbunga Freddy, ambacho huenda kikasababisha mafuriko katika pwani, kinaweza kupita takriban kilomita 120 kaskazini magharibi mwa Mauritius katika sehemu yake ya karibu mapema jioni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.