Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Kusini-mashariki mwa Nigeria: Maafisa watano wa polisi wauawa katika mashambulizi mawili

Maafisa watano wa polisi waliuawa katika mashambulizi mawili Jumapili na Jumatatu na watu wanaoshukiwa kutaka kujitenga kutoka Jimbo la Anambra, kusini mashariki mwa Nigeria, chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi wa urais, polisi imesema.

Afisa wa Polisi aliyejihami kwa silaha akilinda Jumatano hii, Juni 19 katika kituo cha polisi ambapo polisi wawili waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika shambulio la usiku.
Afisa wa Polisi aliyejihami kwa silaha akilinda Jumatano hii, Juni 19 katika kituo cha polisi ambapo polisi wawili waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika shambulio la usiku. BOUREIMA HAMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Raia wa Nigeria wametakiwa kupiga kura siku ya Jumamosi kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari ambaye hatawania kiti cha urais baada ya mihula miwili iliyotawaliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukosefu wa usalama unaoongezeka.

Kusini-mashariki mwa Nigeria ni eneo la machafuko ya watu wanaotaka kujitenga kwa eneo lao, ambao wamefanya mashambulizi mengi dhidi ya polisi na ofisi za Tume ya Uchaguzi (INEC).

Jumatatu asubuhi, watu wanaoshukiwa kuwa wanataka kujitenga "walivamia kituo cha polisi cha Awada katika eneo la Idemilli Kaskazini mwa nchi kwa kutumia vilipuzi vilivyoboreshwa na bunduki za kiotomatiki," msemaji wa polisi katika jimbo hilo, Tochukwu Ikenga amesema.

"Maafisa wanne wa polisi waliuawa," Bw. Ikenga ameongeza katika taarifa, akibaini kwamba washambuliaji watatu pia waliuawa. Sehemu ya kituo cha polisi na magari kadhaa yalichomwa moto katika shambulio hilo, ameongeza. Siku moja kabla, vikosi vya usalama vilizima shambulio lingine, kwenye kituo cha polisi cha Nkwelle-Ezunaka, na kuwaua washambuliaji sita, polisi imesema.

"Wakati wa majibizano ya risasi, afisa wa polisi aliyekuwa kwenye kituo hicho kwa bahati mbaya alijeruhiwa vibaya," amesema Bw. Ikenga. Katika taarifa zake kwa vyombo vya habari, polisi wanahusisha mashambulizi hayo na Vuguvugu la Uhuru kwa Wenyeji wa Biafra (Ipob).

Ipob, ambayo inataka kuuanzisha jimbo lililojitenga kwa kabila la Igbo, imekuwa ikikanusha mara kwa mara kuhusika na ghasia hizo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, zaidi ya maafisa wa polisi 100 na maafisa wengine wa usalama wameuawa tangu mwanzoni mwa mwaka jana katika mashambulizi mbalimbali.

Siku ya Jumamosi asubuhi, watu waliokuwa na silaha walishambulia kituo cha polisi katika eneo la Ogidi katika Jimbo la Anambra, na kuwaua maafisa wa polisi watatu. Mashambulizi kadhaa pia yamerekodiwa katika jimbo hili dhidi ya ofisi za Tume ya Uchaguzi.

Hivi majuzi, IEC ilionya juu ya tishio la kuongezeka kwa ghasia wakati wa kampeni za uchaguzi kote nchini, na kuongeza kuwa imerekodi angalau mashambulizi 50 tangu kuanza kwa zoezi hilo karibu miezi miwili iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.