Pata taarifa kuu
KENYA/ERITREA - DIPLOMASIA

Rais wa Eritrea azuru kenya kwa siku mbili

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki anazuru Kenya kwa siku mbili ambako atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, William Ruto.

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki mjini Mogadishu, tarehe 13 Desemba 2020.
Rais wa Eritrea Isaias Afwerki mjini Mogadishu, tarehe 13 Desemba 2020. AP Photo/Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 77, ambaye amekuwa madarakan tangu mwaka 1993  wakati Eritrea ilipojitenga nha Ethiopia, huwa ni nadra sana atoke nje ya nchi yake.

Mchambuzi wa masuala ya uhusiano wa kimataifa Lee Ndlela akiwa Nairobi nchini Kenya, anaelezea ziara hii na kutoa tathmini kwa nini rais Isaias anazuru Kenya katika kipindi hiki.

Kwa miaka iliyopita hakukuwa na uhusiano mzuri kati ya nchi ya Eritrea na Kenya, kwa hivyo ziara hii ni ya kuimarisha uhusiano wa mataifa haya mawili, marais wakiendelea kushirikiana kutakuwa na usalama na maendeleo. Amesema Ndlela

Rais Afwerki yuko nchini Kenya baada ya mualiko wa mwenzake Ruto, ambaye alitembelea Eritrea mwezi Disemba mwaka jana, miezi mitatu baada ya kuapishwa, kwa lengo la kurejesha uhusiano uliokuwa umeyumba.

Mnamo mwaka 2011, kenya iliituhumu Eritrea kwa kusambaza silaha kwa wanamgambo wa al Shabaab wenye makao yake nchini Somalia.

Katika ziara hii, Afwerki ameandamana na Waziri wa Mambo ya Nje Osman Saleh na Mshauri wa Rais Yemane Ghebreab.

Mara ya mwisho Isaias kutembelea Kenya ilikuwa Desemba 15, 2018.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.