Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi afanya ziara ya kushtukiza nchini Eritrea

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amewasili Eritrea siku ya Alhamisi kwa ziara ya kushtukiza ya siku moja, serikali ya nchi hii katika Pembe ya Afrika kati ya nchi zilizofungwa na za kimabavu zaidi duniani imetangaza.

Peu avant la visite du chef de la diplomatie russe à Pretoria, la Russie et la Chine ont annoncé réaliser des manœuvres militaires près de la côte sud-africaine à l'océan indien. Ici, le ministre russe des Affaires étrangères Sergueï Lavrov lors d'une conférence de presse le 18 janvier 2023.
Peu avant la visite du chef de la diplomatie russe à Pretoria, la Russie et la Chine ont annoncé réaliser des manœuvres militaires près de la côte sud-africaine à l'océan indien. Ici, le ministre russe des Affaires étrangères Sergueï Lavrov lors d'une conférence de presse le 18 janvier 2023. © Alexander Zemlianichenko / AP
Matangazo ya kibiashara

Mheshimiwa Lavrov amekutana hasa na Rais Issaias Afeworki na kujadili "kuimarishwa kwa mahusiano baina ya nchi hizo mbili pamoja na maendeleo ya kikanda yenye maslahi kwa nchi hizo mbili", imesema Wizara ya Habari katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Ziara hii haikuwa katika ajenda ya ziara ya Afrika ya mkuu wa diplomasia ya Urusi, ikiwa ni ziara yake ya pili katika kipindi cha miezi sita katika bara hilo, ambayo hapo awali ilimwona akitembelea Afrika Kusini, Eswatini na Angola.

Ikiongozwa kwa mkono wa chuma na Issaias Afeworki tangu uhuru wake kutoka Ethiopia mwaka 1993, Eritrea ni miongoni mwa nchi tano zilizopiga kura mwezi Machi 2022 dhidi ya azimio la Umoja wa Mataifa la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, pamoja na Urusi, Belarus, Syria na Korea Kaskazini.

Jeshi lake pia linashutumiwa kwa dhuluma nyingi dhidi ya raia katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, ambapo linaunga mkono jeshi la Ethiopia dhidi ya waasi wa Tigray katika mzozo mbaya kati ya mwezi Novemba 2020 na Novemba 2022.

Wanajeshi hawa, waliopo katika eneo hili tangu mwanzo wa vita, walianza kuondoka mwishoni mwa wiki iliyopita, ilitangaza Marekani na serikali ya Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.